Wednesday, June 17, 2020

DAWA YA UTI SUGU






 Maambukizi ya bacteria huweza kuathiri sehemu yoyote ya mfumo huu. Maambukizi ya mfumo wa mkojo ni ya pili ukiangalia maambukizi yote ya mwili.

DALILI ZA MAAMBUKIZI YA MFUMO WA MKOJO.


Dalili hutofautiana kulingana na ukali wa maambukizi,umri na sehemu iliyoathirika.

Dalili zinazojitokeza mara nyingi pakiwa na maambukizi (UTI):

▶Uchungu au kuwashwa unapokojoa.

▶Kuhisi kukojoa mara nyingi.

▶Homa na uchovu .

▶Mkojo wenye harufu mbaya na si safi (cloudy).

DALILI ZINAZOTOKANA NA MAAMBUKIZI YA KIBOFU CHA MKOJO.

▶Maumivu katika upande wa chini wa tumbo.

▶Kukojoa mkojo kidogo , wenye maumivu na mara nyingi.

▶Dalili za homa kidogo. Bila maumivu ya mbavu.

▶Damu kwenye mkojo.


DALILI ZINAZOTOKANA NA MAAMBUKIZI YA UPANDE WA JUU WA NJIA YA MKOJO.

▶Maumivu ya upande wa juu wa mgongo na mbavu.

▶Kuwa na homa na kuhisi kibaridi. Kichefuchefu, kutapika, uchovu na kujihisi mgonjwa kwa ujumla.

▶Kuchanganyikiwa kwa wazee.

🔥Maambukizi haya ni hatari sana yasipotibiwa vyema na haraka. Aidha yanaweza hata kuhatarisha maisha.

Kuwashwa na kukojoa mara nyingi ni dalili za maambukizi ya sehemu za mfumo wa mkojo.

CHANZO CHA MAAMBUKIZI YA MARA KWA MARA YA NJIA YA MKOJO.



➡Kuziba kwa njia ya mkojo.

➡Maumbile ya kike Kwa sababu njia ya yurethra ya wanawake ni fupi kuliko ya wanaume,basi huwezekano wa kupata maambukizi ni mkubwa zaidi kuliko wanaume.

➡Maingiliano/ Kujamiiana: Wanawake wanaoshiriki tendo la ndoa huweza kupata maambukizi mengi zaidi kuliko wenzao wasioshiriki tendo hilo.

➡Mawe Mawe kwenye figo, njia ya kuelekea kwenye kibofu cha mkojo (ureta) au ndani ya kibofu chenyewe yanaweza kuzuia mtiririko wa mkojo na hivyo kusababisha maambukizi.

➡Mpira wa katheta Watu waliowekewa katheta wana uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi kirahisi.


➡Kasoro za kimaumbile Watoto wenye kasoro za kimaumbile kama mkojo kurudi nyuma kama kwenye kibofu na hivyo kwenda kwenye yureta ( vesicoureteral reflux) au kama njia ya yurethra valve inafungukia nyuma, hupata maambukizi kwa urahisi sana.

➡Kuongezeka ukubwa wa tezi dume Wanaume walio na umri wa miaka zaidi ya sitini wanaweza kupata maambukizi kwa sababu ya kukua kwa tezi dume.

➡Kinga ya mwili iliyodhoofika Wagonjwa wa kisukari,UKIMWI au saratani.

➡Sababu nyingine: kama njia za yureta na yurethra kuwa nyembamba,tibi (TB) kwenye njia ya mkojo, neurogenic bladder,diverticulum nk.



_______________________________

Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia

+255758200163

+254743101242

DAR ES SALAM

TANZANIA.

TUWEWAADILIFU USIBADILI CHOCHOTE KWENYE MAKALA HII.

▪️▫️◾️◽️◼️◻️⬛️◻️◼️◽️◾️▫️▪️




Tuesday, June 16, 2020

DAWA YA HEPATITIS B.

DAWA YA HEPATITIS B.

Dawa Asilia ya homa ya ini .
Hii ni dawa inayotibu kabisa ugonjwa wa homa ya ini kwa uwezo wa mola mlezi .

MGONJWA WA HEPATITIS ZIDISHA KULA .

 Vyakula vya baharini (Majini na mtoni {samaki} ) upate omega 3 .

Kula zaidi vitu Asilia visivyo sindikwa.

Tumia chumvi ya mawe epuka au acha chumvi hii ya kawaida.

EPUKA NA ACHA KABISA .

Dawa za kemikali (madawa ya hospitali) pamoja na  pain killers .

Acha pombe kabisa.

Acha soda kabisa

_______________________________

Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia

+255758200163

+254743101242

DAR ES SALAM

TANZANIA.

TUWEWAADILIFU USIBADILI CHOCHOTE KWENYE MAKALA HII.

▪️▫️◾️◽️◼️◻️⬛️◻️◼️◽️◾️▫️▪️

Saturday, June 13, 2020

TATIZO LA KUFA GANZI NA KICHWA KUUMA

KICHWA KUUMA NA KUFA GANZI


SWALI

Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakaat

Naomba ushauri ikitokea kuumwa kichwa tena huwa kama ganzi inaweza kuwa nini hapo.


JAWABU

📛Kichwa kuuma ni dalili ya maradhi mengi sana nani pamoja na hilo la pressure na shida ya macho pia

Miongoni mwa sababu za maumivu ya kichwa

♦️1.maambukizi mwilini mfano malaria,typhoid,maambukizi njia ya hewa n.k

♦️2.damu kuwa nyingi sana au kidogo sana

♦️3.shinikizo la damu

♦️4.presha kuwa chini

♦️5.matatizo ya macho ima ni eye defects au ongezeko la pressure ya macho

♦️6.kuwa na historia ya ajali sehem ya kichwa

♦️7.saratani ya ubongo na nyinginezo

♦️9.maradhi ya figo&inni

♦️10.kutokupumzika ipasavyo (tensions headache)

♦️11.kuwa na uraibu ama dependency ya dawa au vinywaji mfano soda,energy drinks,chai na kahawa

♦️12.msongo wa mawazo
N.k



SWALI LA NYONGEZA

Afwan Dr. hapo katika maelezo yake kuna hali ametaja kufa ganzi kichwa

hii haswa inaashiria nini haswa au nini sababu.

kutakuwa na sababu tofauti ya kufa ganzi au ni pamoja na hayo uliyo eleza?

pia zipo kadhia Dr. mtu amelala kisha kichwa kufa ganzi bila kuuma hii inatokana na nini Dr. Allah akuhifadhi.

JAWABU

🟢Baadhi niliyoyataja hapo juu hupelekea kichwa kufa ganzi kwa baadhi ya watu.

♦️Lakini pia ulalaji mbaya(poor sleeping posture) inaweza sababisha

👉Mfano mtu analalia kifua kwa muda mrefu ni dhahiri kwamba misuli ya shingo yake haiwi katika hali ya utulivu (relax) itakua ni yenye kujivuta upande mmoja zaidi ikitokeze mishipa ya upande mmoja haipeleki damu sawasawa kama inavyo takiwa basi mtu anaweza pata chamgamoto hiyo ya ganzi na misuli ya shingo kuwa na maumivu
Lakini si kila anaepata ganzi basi alilala vibaya laa!


Suluhu ni kuzishulikia sababu na si matokeo pekee kwa maana ukawa ni mtu wa kula dawa za maumivu kila siku


..✍ MTOA MAJAWABU
DR. ABUU HUDHAIFAH حفظه الله



Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia

+255758200163

+254743101242

DAR ES SALAM
TANZANIA.



🔴TUWEWAADILIFU USIBADILI CHOCHOTE KWENYE MAKALA HII.

▪️▫️◾️◽️◼️◻️⬛️◻️◼️◽️◾️▫️▪️

Friday, June 12, 2020

HABAT SAUDAA DAWA YA MAGONJWA MENGI

DAWA YA MAGONJWA MENGI HABAT SAUDAA.




1⃣. MATATIZO YA TUMBO.

Mafuta ta habat saudaa kijiko kimoja  changanya na juice ya Tangawizi kijiko  kimoja kunywa  1x3 


2⃣. HEDHI KUTOKA CHACHE .

Changanya unga wa habat saudaa na Asali kunywa kwa maziwa moto x2 kwa siku

3⃣. KUFURA.

Sugulia mafuta ya habat saudaa sehemu iliyovimba iache sehmu hiyo masaa 5 ndipo uoshe .


4⃣ KIPANDA USO.

Paka mafuta ya habat saudaa kwenye paji la uso 

5⃣ UCHOVU.

Chemsha kijiko kimoja cha habat saudaa kwa moto mdogo kisha changanya na ndimu kunywa 1x1 .


6⃣ UPARA.

Changanya mafuta ya habat saudaa na mafuta ya nazi . Sugulia kwenye upara na nywele kila baada ya kuoga .

7⃣. HOMA.


Changanya mafuta ya habat saudaa na juice ya chungwa kwenye maji vuguvugu changanya kunywa x2 kwa siku.



8⃣. MINYOO.


Siki ya Apple vijiko viwili changanya kijiko kimoja cha mafuta ya habat saudaa. Kunywa vijiko viwili vya chakula X2 kwa siku.



9⃣. MENO KUUMA.


Sugulia mafuta ya habat saudaa  kwenye meno yanayo uma na fizi .


🔟. KUKOSA USINGIZI.


Changanya Asali kijiko cha chai na  nusu kijiko cha chai mafuta ya habat saudaa changanya vyote kwenye kikombe cha maji moto kunywa wakati wa kulala .


1⃣1⃣. PUMA .


Changanya kijiko cha chai cha mafuta ya habat saudaa na mafuta ya nanaa kwenye maji yanayochemka vuta mvuke wake kwa dk 20 .


1⃣2⃣. UGONJWA WA NGOZI.


Changanya unga wa habat saudaa , Unga wa Sulfa na mafuta ya ufuta . pakaa sehemu zilizo athirika.


1⃣3⃣. KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA.


Ujazo sawa Asali na mafuta ya habat saudaa kunywa kijiko cha chai kabla kula chochote .



1⃣4⃣.  MBA.


Changanya mafuta ya habat saudaa kijiko cha chai , Unga wa sulfa kijiko cha chai, Vijiko vitatu vya unga wa hinna vipashe kwa moto mdogo dk 5 iache ipoe kisha pakaa sehemu zilizo na mba.


1⃣5⃣. KUVIMBIWA.


Habat saudaa kijiko cha chai vijiko viwili  shamari , Vijiko viwili vya Asali changanya kwa maji moto kunywa x2 kwa siku .



1⃣6⃣. HEDHI KUKOMA.


Bugia Habat saudaa vijiko viwili vya chai kila siku .




IMEANDLLIWA NA ABUU AJMI حفظه الله




________________________________


Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia

+255758200163
+254743101242

DAR ES SALAM
TANZANIA.




Thursday, June 11, 2020

DAWA YA FANGUSI




FUNGASI NI NINI ?


MWANDIAHI; DR. ABUU ABAYDULLAH حفظه الله


✍🏽Mapunye ni ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na fungus jamii ya Tinea.

👉🏽Jamii hizi za fungus hupewa majina kutokana na sehemu ya ngozi inayoshambulia
Mathalani pindi zinaposhambulia;
◼-Kichwani yaitwa Tinea capitis
◼-Mwilini naitwa Tinea corporis
-Sehemu za siri yaitwaTinea pubis
◼-Katikati ya vidole vya miguu yaitwa Tinea ungium.


💢Muonekano wake;


🔴Za kichwani na mwilini huwa zinakaribia kuwa sawa, huwa zinaanza kuwa na mduara uliotengenezwa na vijipele vyekundu .

Vya katikati ya vidole huwa ni utando mweupe ulio katikati ya vidole( mara nyingi kutokea kwenye vidole vya mwisho ambavyo vimeshikana kiasi cha kukosa nafasi)


DALILI ZA FUNGUS ZA MWILINI (TINEA)


 🔴Tinea capitis na corporis na pubis :
👉🏽uwepo wa mapunye +/- muwasho wa sehemu husika , 
👉🏽kutoa maji maji sehemu husika au kutunga usaha( hapo itaashiria na uwepo wamashambulizi ya baccteria)

Tinea ungium; huwa ni uwepo wa huo utando+/- muwasho wa sehemu husika na harufu mbaya katikati ya vidole.

MATIBABU YA HOSPITALI


👉🏽tunatoa topical anti fungals kama Whitefield cream( huwa inakawaida ya kuwasha ila ni nzuri) na miconazole cream. Pia na ant biotics kama mupurocin cream kama kutakuwa na bacteria infection.

USHAURI/JINSI YA KUJIKINGA


💧Jitahidi suala la usafi yaani kuoga angalau mara 2 kwa siku na sabuni( kwa fungus za mwilini na kichwa),

Kujitahidi kukausha majimaji yanayobakia katikati ya vidole.



✍🏽NYONGEZA KUTOKA KWA DR. ABUU HUDHAIFAH حفظه الله



Kwa kuongezea katika maelezo ya daktari hapo juu ni kwamba fungus ni kitu nyemelezi na vinapopatikana mazingira rafiki basi hujitokeza;

🍀1.kinga ya mwili kuwa chini mfano kwa kisukari,saratani, virusi vya ukimwi,matumizi makubwa ya dawa aina za steroid na antibiotic ,

🍀2.Mazingira ya unyevu unyevunyevu,
🍀3.Kutokutumia dawa za fangus kwa kipindi kinachotakiwa ,
🍀4.kutokufata maelekezo ya namna ya kutibu sababu ya awali primary cause.


BARAKAALLAHU FIYKUM





DAWA ASILIA ZA FUNGUS ZA MIGUU.






1⃣ UNGA WA MAJANI YA MPERE

Unga wa majani ya mpera changanya na maji kidogo . Paka katikati ya vidole vilivyo na fungasi (twanga unga uwe laini sana ).

2⃣KITUNGUU SAUMU NA MAFUTA YA ZAITUN .

Twanga vitunguu saumu kisha vitie katika maji vuguvugu loweka miguu nusu saa .


👉Twanga vitunguu saumu viwe rojo laini changanya na mafuta ya zaytuni ujazo sawa .


pakaa katika katika ya vidole x3 kwa siku .


👉Tafuna punje 3 za vitunguu saumu asubuhi kabla hujala chohote na tia vitunguu saumu katika mapishi ya mlo wako.



DAWA NA ABUU AJMI حفظه الله

_______________________________

Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia

+255758200163

+254743101242

DAR ES SALAM
TANZANIA.



🔴TUWEWAADILIFU USIBADILI CHOCHOTE KWENYE MAKALA HII.

▪️▫️◾️◽️◼️◻️⬛️◻️◼️◽️◾️▫️▪️

Wednesday, June 10, 2020

PTOSIS

UGONJWA PTOSIS
_______________________


Ptosis ni hali hutokea kigubiko cha juu cha jicho au macho yote hushuka.

Ushukaji unaweza kuwa mdogo usiodhirika mpaka atizame kwa kiyoo au unaweza kuwa mkubwa anao uhisi sana au  kuwa mkubwa hata kuzui kuona.



Kushuka kwa kigubiko cha jicho hutokea kwa sababu misuli ya levator (misuli inahusika na kunyanyua na kushusha kigubiko cha jicho) Imeadhirika.


ZIPO AINA SITA ZA PTOSIS.
_________________________


1. APONEUROTIC PTOSIS. 

Hii ndiyo hali maarufu zaidi ambayo inahusishwa na kuzeeka.

Misuli ya levator inakuwa imetumika sana na haina uwezo wa kujirudisha kama ilivyofanya awali.

Hali hii inaweza sababishwa na kupikicha jicho sana au matumizi ya lensi muda mrefu.

2. NEUROGENIC PTOSIS.


Hali hii hutokea njia za  nerves zinazo dhibiti harakati za kigubiko cha jicho zimeharibika.

hali hii inaweza sababishwa na Horner syndrome, third nerve palsy, au myasthenia gravis.


3. MYOGENIC PTOSIS.

Hali hii hutokea maradhi yanayo athiri mifumo ya mwili kama mafua na shinikozo la damu,Kisukari husababisha udhaifu wa misuli kama udhaifu wa mshikamano wa misuli.

Hali hii huchangia pia kutokana na misuli mingine mwilini kuendelea kudhofika, wakati mwingine hata misuli ya levetor.




4. MECHANICAL PTOSIS.

Kama kigubiko cha jicho kimelemewa na mkandamizo uliozidi wa ngozi Mechanical ptosis inaweza kutokea.

5. TRAUMATIC PTOSIS

Ptosis inaweza kutokana na majeraha au maumivu ya ndani ya kigubiko cha jicho au jicho .

Hali hii hutokana na kutokuvaa vizuizi vya macho wakati wa kazi zinazohitajia hivyo kama uchomeleaji au baadhi ya michezo inayo inayohitaji kuvaa vizuizi.

6. CONGENITAL PTOSIS.

Watoto wanaweza kuzaliwa na kigubiko cha jicho kilichoshuka.

Hali hii hutokea misuli ya levetor haijakuwa vizuri katika fuko la uzazi.

Imtokeapo mtoto hali hii inabidi afanyiwe vipimo na tiba ya haraka. Kadri mtoto anavyokuwa hali hii inazidi kuwa mbaya.

Tuesday, June 9, 2020

JINSI YA KUMNYONYESHA MTOTO

NJIA BORA YA KUNYONYESHA MTOTO.

Namna ya kunyonyeaha mtoto


🌹1.Hakisha mama amekaa kitako akiwa amegemea na awe na utulivu

🌹2.Mtoto alale juu ya sehem ya mbele ya mkono wa mama katika upande wa ziwa analotaka kunyonyoshwa huku kiganja cha mama kikishika makalio ya mtoto. Mfano mtoto ananyonyeshwa ziwa kushoto basi mtoto ashikiliwe na mkono wa kushoto

🌹3.Mtoto amuelekee mama huku tumbo la mama na la mtoto yakiwa yamegusana

🌹4.Sehemu nyeusi ya ziwa la mama iwe kwenye kinywa cha mtoto na Si chuchu pekee

🌹5.Ziwa la mama alishike kwa vidole vyake vinne katika sehem ya chini ya ziwa na kidole gumba kiwe juu

🌹6.Hakikisha kuwe na utulivu wakati wa kunyonyesha

🌹7.Mtoto awekwe begani baada ya kunyonyeshwa
NB:Ni kosa kunyonyesha mtoto huku mama akiwa amelala chini. 

Mtoto anyonyeshwe maziwa ya mama bila ya kuongezewa kitu chochote katika miezi 6 ya mwanzo.


..✍Mwandishi DR. ABUU HUDHAIFAH حفظه الله




Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia

+255758200163

+254743101242

DAR ES SALAM
TANZANIA.

🔴TUWEWAADILIFU USIBADILI CHOCHOTE KWENYE MAKALA HII.

▪️▫️◾️◽️◼️◻️⬛️◻️◼️◽️◾️▫️▪️

Monday, June 8, 2020

DAWA PERA YA MARADHI MENGI

DAWA PERA (MAJANI).





HARUFU MBAYA YA KINYWA NA VIDONDA VYA MDOMNI (MOUTH ULCER).

Chemsha majani sita ya mpera dakika 10 sukutua kwayo .



MABAKA YA CHUNUSI (BLACK HEAD /MAKOVU YATOKANAYO NA MAJERAHA).

Saga majani ya mpera na maji kidogo sugulia sehemu zilizo athirika 


KUFUNGA KUHARISHA .

Chemsha majani ya mpera  kwa maji vikombe 4 kwa dk 5 kunywa nusu glass x5 kwa siku.


KUONDOA UKURUTU (ECZEMA).

Changanya unga wa majani yaliyo kauka ya mpera na maji kidogo pakaa sehemu zenye ukurutu. 1x2 siku 10


KANG`ATWA NA MDUDU.

Kamulia majani ya mpera mabichi sehemu uliyo ng`twa.


KUHARA DAMU (DYSENTARY),KUKOSA CHOO, TUMBO KUJAA GESI NA KUVURUGIKA TUMBO.

Chemsha mizizi na majani ya mpera kunywa kikombe moja  1X3 kila siku .



MAUMIVU YA VIUNGO (ARTHRITIS ).

Twanga majani ya mpera tia maji kidogo paka  sehemu zenye maumivu .


FUNGUSI ZA MIGUUNI.

Unga wa majani ya mpera changanya na maji kidogo . Paka katikati ya vidole vilivyo na fungasi (twanga unga uwe laini sana ).


UGONJWA WA FIZI.

Chemsha majani ya pera , Chumvi ,Pilipili manga (unga ) kwa dakika 5 sukutua x2 kwa siku .

KUTOONA VIZURI.

Kunywa glass moja ya majani ya mpera kila siku kwamwezi moja .


IMEANDLLIWA NA ABUU AJMI حفظه الله




________________________________


Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia

+255758200163
+254743101242

DAR ES SALAM
TANZANIA.

HUKMU YA KUPANDIKIZA MIMBA .


اَلسَلامُ عَلَيْكُم وَرَحْمَةُ اَللهِ وَبَرَكاتُهُ‎‎


Afwan mwalimu wetu mbora , Tunaomba tusaidie kuhusu jambo hili la kupandikiza mimba katika kizazi je mwalimu wetu mbora inafaa kufanya hivyo ?


kama inafaa zipi sharti  zake?

BarakaAllahu fiyka .

JAWABU ;
Sheikh Abū Ayman bin Akida Dhahiir Al-Shiiraaziy Al-Shāfi'iyy حفظه الله

 وعليكم السلام ورحمة الله وبركاته

 Jambo hili ni jambo la khatari sana kama walivyosema 'Ulamaa, na limekaliwa na tume ya Fiqh kule Makkah, wakatoa tija ambayo naifupisha ifuatavyo

Kama mke wamethibitisha Madaktari wahusika kuwa ni tasa basi haifai kufanya hiyo amaliyyah.


Kama mke si tasa ila ana hitlafu fulani inayosababisha kutokufika manii ya mumewe mahala panapostahiki basi amaliyyah hiyo itafaa kwa sharti mume mwenyewe ndo amkabidhi Dr wa kike manii yake ili amuwekee mwanamke mahala husika, akikosekana Dr wa kike basi mwanaume atakuwa ni nambari mbili kwa maana baada ya kukoseKana nambari moja ambaye ni wakike. 

Na hiyo amaliyyah ifanyike wakiwepo watu watatu tu, mume lazima ashuhudie, mke mfanyiwa amaliyyah  hiyo pamoja na Dr atakayemuweka hizo mbegu.

Pamoja ya ruhusa hiyo ila bado wanasema 'Ulamaa awla ni kuacha kufanya hivyo japo hawajaharamisha.

Nimetohoa hayo kutoka katika fat'wa ya 'Allāmah bin Baaz (Allāh amrahamu).



JAWABU;  Sheikh Abū Ayman bin Akida Dhahiir Al-Shiiraaziy Al-Shāfi'iyy حفظه الله






Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia

+255758200163
+254743101242

DAR ES SALAM
TANZANIA.





Sunday, June 7, 2020

DAWA YA KUSHUSHA HARAKA

EWE DADA MAPISHI SIO KUWASHA MOTO TU, JIFUNZE KUMPA MUMEO VITU FRESH VYENYE KUAMSHA HISIA ZA TENDO LA NDOA NA KUMPA NGUVU ZA KUKUFIKISHA PATAMU ZAIDI.


➡Kushusha haraka bila kutaka ni tatizo linalowakumba wanaume wengi hata mara nyingine hutokea kabla dhakari haijaingia ukeni au kumwaga mapema iingiapo ukeni dakika chache dk 2 , 3 kwishnei. (He reaches a point of no return )

MWANDALIE DAWA HII BIIDHINILLAH NDOA ITAKUWA TAMU .


MAHITAJI .






▶LIMAO 6,
▶TIKITI MAJI ¼  , 
▶NDIZI 2,
▶TANGAWIZI 3,


MAANDALIZI .

BLEND VYOTE PAMOJA.

MATUMIZI .


KUYWA KILA SIKU KADIRI YA UWEZO WAKO.



KARIBU UJIPATIE RIJALI EXTRA DAWA MUJARAB BIIDHINILLAH KWA TATIZO LA KUWAHI KUSHUSHA.




shuda wa Rijali extra ⤴


IMEANDALIWA NA ABUU AJMI حفظه الله


Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia

+255758200163
+254743101242

DAR ES SALAM
TANZANIA.




Saturday, June 6, 2020

DAWA YA VIDONDA VYA TUMBO.

UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO

Ugonjwa wa Vidonda vya tumbo (peptic ulcers ), au madonda yanayotokea katika tabaka la tumbo au kwenye duedenum (sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba ), huwa vikali sana na vinauma mno .

Kawaida maumivu na uchungu wa peptic ulcer hutambulika kama maumivu ya tumbo mara nyingine husababisha maumivu ya kifua .

SIFA ZA MAUMIVU.

Maumivu yanayo zalishwa na peptic ulcer yanatambulika kwa kuunguza (burning) au kuwaka moto .

Maumivu huzidi mara ulapo chakula au huzidi zaidi unapokula baadhi kama kunywa  kahawa , pombe, kutafuna gums , kuvuta sigara .

Maumivu yanaweza kuambatana na Gesi tumboni , kichefuchefu, kutapika na kiungulia .

CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO . (PEPTIC ULCERS ).

Vidonda vya tumbo vinaweza kutokea wakati ute /kamasi au utelezi unaolinda sehemu ya juu ya utumbo imepungua au uzalishaji wa acidi tumboni kuongezeka .

Hali zinazo sababisha mara nyingi vidonda vya tumbo (peptic ulcers ) kwa watu wengi ni njia za usagaji wa chakula kutawaliwa na bakteria helicobacter pylori . Na pia matumizi ya NSAID (dawa) za kutuliza maumivu huzidisha uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo (peptic ulcers).



UHUSIANO KATI YA VIDONDA VYA TUMBO NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UGUMBA.

✍ Helicobacter Pylori (H. Pylori) ni bakteria ambaye hushambulia sehemu ya mwisho ya tumbo la chakula ( gastro ) na sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo ( duodenum ) ijulikanayo kama ( grastoduodenal tract ) na kupelekea tatizo la vidonda vya tumbo ( peptic ulcers ) na huyo bakteria watu humpata kupitia matumizi ya maji, vyakula na vyombo vyenye huyo bakteria kutokana na kutokusafishwa ipasavyo.

Maambukizi ya H pylori hayaishiitu katika sehemu ya mwisho ya utumbo mkubwa na sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo ( gastroduodenal tract ) bali husababisha mpaka magonjwa mengine ndani na nje ya mfumo wa chakula.

Kutokana na utafiti uliofanywa ulionesha H pylori anauwezo wa kusababisha magonjwa nje ya mfumo wa chakula kama magonjwa katika
➡Moyo
➡Mishipa ya damu
➡Kolomeo
➡Ngozi
➡Mfumo wa hewa
➡Mfumo wa homoni
➡Mfumo wa kinga ya mwili
➡Mfumo wa utengenezaji wa damu
➡Mfumo wa ubongo na utiwa wa mgongo.

Hivi karibuni ushahidi kutokana na utafiti umeonesha kuwepo ongezeko la tatizo la ugumba kwa wanaume na wanawake wenye H pylori zenye gene iitwayo CagA kulinganisha na wale ambao hawana H pylori

Kupitia njia mbali mbali H pylori mwenye gene CagA huweza kuchochea uzalishaji wa vichochezi vya inflammation na kinga za mwili ambazo huweza kuathiri moja kwa moja ama kwa njia nyingine mfumo wa uzazi.

Kwa wale watu wenye Vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na
H Pylori zenye gene ya CagA huweza kupelekea uharibifu wa mbegu za uzazi kwa wanaume na wananawake kwa kupunguza uwezo wa hizo mbegu kusafiri ( low motility), kuwa na nguvu na ustahimilivu (low vitality) ama uharibifu wa muonekano wa hizo mbegu
( Sperm cell morphology destruction )

Na huu uharibifu wa hizi H pylori haujajulikana unakuwaje bali inadhaniwa inaweza kuwa kwa njia mbili kwa upande wa wanaume;

A- kwa kuchochea kinga za mwili ambazo hushambulia kuta za seli ambazo huzalisha mbegu za kiume

B- kwa kuchochea mwili kuzalisha vichochezi ( inflammatory mediators ) kama interleukin na necrosis factor ambazo huenda na kushambulia mbegu za kiume.

Na kwa upande wau wanawake mapendekezo ni mengi ila inadhaniwa H pylori mwenye gene CagA huweza kuchochea uzalishaji wa kinga za mwili ambazo hupelekea mabadiliko katika mji wa uzazi ( uterus ) ambayo huathiri taratibu za Mbegu za kiume kuungana na yai la mwanamke.

Kutokana na tafiti hizo inaonesha vidonda vya tumbo husasababisha upungufu wa nguvu za kiume na uwezo wa mwanamke kupata mimba.

Ni dhahiri kwa wanaosumbuliwa na vidonda vya tumbo huweza kupungukiwa nguvu za kijinsia na kupelekea;

1. kukosa hamu ya tendo la ndoa
2. Kushindwa kufanya tendo la ndoa
( kwa wanaume )
3. Uume kuwa legelege kutokana na athari za vidonda vyatumbo
( kwa wanaume )
4. kushindwa kushika au kutungisha mimba

Hivyo basi kwa wale wenye vidonda vya tumbo ni vyema kutibu chanzo hiki kabla ya matumizi ya dawa za uzazi.

Tumia Shifaa Dawa ya vidonda vya tumbo.







VITU VYA KUEPUKA KWA MWENYE VIDONDA VYA TUMBO




🔥Epuka Chumvi nyingi kwenye mlo
🔥Epuka Mafuta mengi kwenye mlo
🔥Epuka kula Nyama nyekundu (Ng`ombe, Mbuzi , Kondoo n.k)
🔥Epuka matumizi ya Tangawizi , pilipili manga
🔥Epuka kula Nanasi ,Fenesi
🔥Epuka kunywa Maziwa
🔥Epuka kula Machungwa , Limao ndimu
🔥Epuka kula Maharage na vyakula vyote unapokula tumbo linajaa gesi viepuke .
🔥Epuka Kutafuna gum, (Big G bablish,ballgum, pk n.k)
🔥Epuka ugali wa sembe)




________________________
VITU VYA KUACHA KABISA


❌Acha kunywa Pombe
❌Acha Kunywa Soda (Carbonated   beverages).
❌Acha kuvuta Sigara
❌Acha kula miraa







MWANDISHI ....✍ ABUU NAWFAL MZAMIRU KATUNZI NA ABUU AJMI 

Rejea;-

1. World Journal of Gastroenterology.
8226 Regency drive ,Pleasanto, CA 94588, USA ©2014

2. Wei Wu1, Qiuqin Tang2, Hao Gu1, Yiqiu Chen1, Yankai Xia1, Jiahao Sha3 and Xinru Wang1 Address all correspondence to: wwu@njmu.edu.cn; xrwang@njmu.edu.cn

1 State Key Laboratory of Reproductive Medicine, Department of Toxicology, School of Public Health, Nanjing Medical University, Nanjing, China

2 State Key Laboratory of Reproductive Medicine, Department of Obstetrics, Nanjing Maternity and Child Health Care Hospital Affiliated to Nanjing Medical University, Nanjing, China

3 State Key Laboratory of Reproductive Medicine, Nanjing Medical University, Nanjing, China

WASILIANA NASI KWA DAWA NZURI YA VIDONDA VYA TUMBO NA NGUVU ZA KIUME.

________________________________


Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia

+255758200163
+254743101242

DAR ES SALAM
TANZANIA.


jiunge chanel yetu kwa masomo mbalimbali ya tiba Asilia





Friday, June 5, 2020

UTASA




UTASA.


AINA ZA UTASA.


UTASA KWA MWANAMUME.


Utasa upo aina mbili:

▪Kwanza: UTASA WA KIUNGO:

Hutibiwa kwa madaktari kama wakiweza kuutibu


▪PILI; UTASA KWA SABABU YA MGUSO WA JINI NDANI YA MWILI WA MWANADAMU.

Hutibiwa kwa Quran dua na nyurad.

▪️Yafahamika kuwa, utendaji wa kuzalisha -kwa idhini ya Allahﷻ -ni kiwango cha wadudu wa manii kwa mwanamume wawe ni zaidi ya milion ishirini (20000000/=). katika sentimita za mraba.

Mara nyingine shetani huwa akiyabana mapumbu ya mwanamume yanayotoa wadudu wa manii, au huwa akitumia njia nyingine mapumbu hayo yakatoa kiwango kidogo chini zaidi ya itakiwavyo, ikawa ndio sababu ya kutozalisha.

Wakati wadudu wa manii wanapogura kutoka katika  mapumbu hadi katika kibofu cha manii, wadudu hawa huhitajia kiowevu cha ute kinachotolewa na tezi ya koubar na kuimimina katika kibofu cha manii wakati ambapo wadudu hawa waliohifadhiwa katika kibofu hiki huwa wakiila.

Na hapa shetani huwa ana tabia nyingine katika tezi hiyo ya koubar, huwa akiizuwia kutoa kiowevu cha ute, hapobasi wale wadudu waliohifadhiwa katika kibofu cha manii hawapati chakula, basi huwa wakifa na ikawa vigumu mtu kuzaa.




UTAFAUTISHAJI BAINA YA UTASA WA KIMAUMBILE NA UTASA ULIOSABABISHWA NA JINI.


DALILI ZA UTASA ULIONASIBISHWA NA JINI.

1. Kuhisi dhiki kifuani hasa baada ya Alasiri, na pengine huendelea hadi katikati ya usiku.

2. Kutokuwepo kiakili na usahaulifu.

3. Kuhisi maumivu chini ya pingili la uti wa mgongo.

4. Wasiwasi na hamaniko usingizini.

5. Usingizini mwake huwa akiona ndoto za kutisha.


UTASA KWA MWANAMKE;

vilevile utasa kwa mwanamke upo aina mbili


1. UTASA WA KIMAUMBILE.
hivi ndivyo alivyoumbwa na Allah awe tasa.

2. UTASA ULIOSABABISHWA NA JINI ALIYESTAKIRI KATIKA KIZAZI CHA MWANAMKE, KWA NAMNA YA KUYAHARIBU MAYAI, NA HAPO ISIWEZEKANE KUZAA.

Au JINI atamwacha mpaka mimba ikamilike, lakini baada ya miezi kadhaa ya mimba, shetani huukanyaga mshipa katika kizazi cha mwanamke damu ikateremka na ikasababisha kuavya (kuharibu mimba).

Mara nyingi kuavya kunakaririwa huwa kumesababishwa na jini.

Hali nyingi za aina hii zimetibiwa.  Imethubutu katika Sahihul-Bukhari na muslim kuwa shetani hupita ndani ya mwanaadamu mapito ya damu.

Bukhari 4/282 fat-hi) na Muslim ( 14/155 Nawawy).




rejea Kitabu; 
الصرم البتارفي التصدي السحرة الأشرار

Mwandishi; Shaykh Wahid Abdus Salam Bali.

Mfasiri; Ustadh Uthman Muhammad Ali.


DAWA YA UGUMBA /UTASA KWA UWEZO WA MOLA MLEZI .


Ni vizuri hali hii mume na mke wahudhurie hospitali wafanyiwe uchunguzi na Daktari bingwa .

 Hali ikiwa imeambatana na dalili za sihiri waone wasoma Ruqya ya kisheria waweza kuitengua kwa uwezo wa Allahu hiyo sihiri .


TUMIA DAWA HII KUJITIBIA UTASA .



Asali lita moja ,
Mdalasini nusu kilo ,

 Changanya vizuri kunywa ujazo wa kikombe cha kahawa 1 X3 kila siku 
anywa mume na mke a kumuomba mola mlezi awaruzuku mtoto .

KWA MAHITAJI YA DAWA NZURI YA CHANGO LA UZAZI WASILIANA NASI UIPATE RIJALI EXTRA ZAWADI KWA WANANDOA.






Mwandishi Abuu Ajmi حفظه الله 




_____________________________________


Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia


+255758200163

+254743101242


DAR ES SALAM

TANZANIA.



🔴TUWEWAADILIFU USIBADILI CHOCHOTE KWENYE MAKALA HII.


▪️▫️◾️◽️◼️◻️⬛️◻️◼️◽️◾️▫️▪️






DAWA YA BAWASIRI

HERMORRHOIDS KEY .

dawa ya bawasiri.


HI NI DAWA INAYOTIBU BAWASIRI AINA ZOTE YA NDANI NAYA NJE KWA UWEZO WA MOLA .



DALILI ZA BAWASIRI ZINATEGEMEA NA AINA YA BAWASIRI.



1⃣BAWASIRI YA NJE.

Hutokeza nje ya ngozi inayozunguka dubri .

⭕Kuwashwa au kuwasha eneo  linalozunguka dubri,

⭕Maumivu yenye kukera na kusumbua,

⭕Kiuvimbe kilicho tuna nje ya dubri,

⭕Kuvuja damu ,


  • 2⃣BAWASIRI YA NDANI .

Bawasiri ya ndani  ya utumbo wa mwisho karibu na dubri. Huwezi kuiona au kuihisi na mara chache husababisha usumbufu. Lakini kukaza au kuwasha wakati wa kupitisha haja kubwa kunaweza kusababisha ;


⭕Damu kutoka bila maumivu wakati wa kukidhi haja kubwa . Unaweza kuino kwenye choo au karatasi ya kujifutia (Tissue paper )

⭕Bawasiri (kinyama ) kutokeza kwenye dubri na kusababisha kuwashwa na maumivu.




3⃣Thrombosed hemorrhoids.


Kama damu itatuama katika bawasiri ya nje na kuganda (thrombus ), itasababisha-;

⭕Maumivu makali ,

⭕Kufura ,

⭕Uvimbemchungu wenye kuwasha ,

⭕Kivimbe kigumu kwenye dubri.


VISABABISHI VYA BAWASIRI.

Mishipa karibu na dubri huwa inajinyoosha kwa nguvu na kupanuka au kuvimba.  Bawasiri inaweza  kukua kutokana na shinikizo kubwa kwenye mfereji wa chini kutokana na -;

🔹Kujikaza wakati wa haja kubwa ,

🔹Kukaa muda mrefu wakati wa haja kubwa ,

🔹Kuharisha sana au kupata choo kwa tabu kama cha mbuzi, 

🔹Ujauzito ,

🔹Kufanywa liwati kuingiliwa tundu la haja kubwa dubri,

🔹Kuinua mara kwa mara vitu vizito(sana ),

🔹Kunenepa sana,

🔹Ulaji wa vyakula visivyokuwa na kamba kamba/nyuzi (fibre).

Kadiri unavyozeeka, hatari ya kupata bawasiri inaongezeka .Kwa sababu tissue zinazo shikiza mishipa kwenye mreji na dubri zinaweza kuchoka na kulegea .

Hii inaweza tokea kwa mjazito , kwa sababu uzito wa mtoto hukandamiza eneo lote la dubri.


JINSI YA KUJIKINGA NA BAWASIRI .


🍀Kula vyakula vyenye nyuzi nyingi kama makoma ,

🍀Kunywa maji yakutosha,

🍀Usijikaze sana wakati wa haja kubwa,

🍀Jisadie haraka pindi unapohisi haja kubwa , ukichelewa kutoa kinyesi kinarudi na hisia hupotea , Choo kitakuwa kikavu na kigumu hata kushindwa kukitoa kutoka ,

🍀Fanya mazoezi ,

🍀Epuka kukaa chini sana . kukaa muda mrefu , haswa chooni kunaweza zidisha msukumo mkubwa wa mishipa kwenye dubri .





Mwandishi Abuu Ajmi حفظه الله 




_____________________________________


Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia


+255758200163

+254743101242


DAR ES SALAM

TANZANIA.




🔴TUWEWAADILIFU USIBADILI CHOCHOTE KWENYE MAKALA HII.


▪️▫️◾️◽️◼️◻️⬛️◻️◼️◽️◾️▫️▪️








Thursday, June 4, 2020

DAWA YA VIDONDA VYA TUMBO

SHIFAA  




HII NDIYO DAWA YA VIDONDA  VYA TUMBO KWA UWEZO MOLA MLEZI.







SHIFAA.

DAWA YA VIDONDA VYA TUMBO .

INATIBU KWA UWEZO WA ALLAHU MAUMIVU NA DALII ZOTE ZA VIDONDA VYA TUMBO KAMA ,

TUMBO KUJAA GESI,
TUMBO KUWAKA MOTO,
TUMBO KUUMA,
KUHARISHA,
KUPATA CHOO KIGUMU,
MGONGO NA KIUNO KUUMA NA KUWAKA MOTO,

KUKOSA HAMU YA KULA,
DAWA INASAIDIA USAGANI WA CHAKULA NA KUTIBU VIDONDA VYA TUMBO KABISA BIIDHINILLAH .


WASILIANA NASI SUBIRA TIBA ASILIA

+255 758200163.
+254 743101242.

HIZI NDIZO NAMBA RASMI ZA SUBIRA TIBA ASILIA .




VITU VYA KUEPUKA KWA MWENYE VIDONDA VYA TUMBO






🔥Epuka Chumvi nyingi kwenye mlo
🔥Epuka Mafuta mengi kwenye mlo
🔥Epuka kula Nyama nyekundu (Ng`ombe, Mbuzi , Kondoo n.k)
🔥Epuka matumizi ya Tangawizi , pilipili manga
🔥Epuka kula Nanasi ,Fenesi
🔥Epuka kunywa Maziwa
🔥Epuka kula Machungwa , Limao ndimu
🔥Epuka kula Maharage na vyakula vyote unapokula tumbo linajaa gesi viepuke .
🔥Epuka Kutafuna gum, (Big G bablish,ballgum, pk n.k)
🔥Epuka ugali wa sembe)




________________________
VITU VYA KUACHA KABISA


❌Acha kunywa Pombe
❌Acha Kunywa Soda (Carbonated   beverages).
❌Acha kuvuta Sigara
❌Acha kula miraa




MWANDISHI ABUU AJMI HUSSEINحفظه الله









__________________________________________

Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia

+255758200163
+254743101242

DAR ES SALAM
TANZANIA.


🔴TUWEWAADILIFU USIBADILI CHOCHOTE KWENYE MAKALA HII.

▪️▫️◾️◽️◼️◻️⬛️◻️◼️◽️◾️▫️▪️


DAWA YA KISUKARI.

DAWA YA KISUKARI TYPE 2.






MAHITAJI,

MAJANI YA MPERA KIGANJA KIMOJA
MANJANO KIPANDE KIMOJA 


CHEMSHA DAKIKA 10 KWA MAJI LITA MOJA .

ACHA IPOE 

KUNYWA GLASS MOJA ASUBUHI MCHANA NA JIONI .


DOZE MIEZI 6.


UNAEZA KUITUMIA KAMA KINGA KWA KUINYWA KILA SIKU 1X1 KWA WALE HAWANA KISUKARI .



Mwandishi Abuu Ajmi حفظه الله 




_____________________________________


Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia


+255758200163

+254743101242


DAR ES SALAM

TANZANIA.



🔴TUWEWAADILIFU USIBADILI CHOCHOTE KWENYE MAKALA HII.


▪️▫️◾️◽️◼️◻️⬛️◻️◼️◽️◾️▫️▪️






Wednesday, June 3, 2020

SIHIRI /UCHAWI /KIJICHO.

SIHIRI/UCHAWI AU KIJICHO.
                



Amesema Ibnu Qudama Al Maqdisy; 
Sihiri(uchawi) ni kifundo, zunguo na maneno yanayosemwa au kuandikwa, au afanye jambo litakaloathiri katika mwili wa aliyesihiriwa au moyoni mwake au akilini mwake bila  ya kumshika.  Nayo ina uhakika, Kuna yenye  kuuwa, yenye kutia maradhi, inayomzuia mwanaume asiweze kumjamii mkewe. Muna na inayomtenganisha mtu na mkewe na inayomchukiza mmojawapo kwa mwenzie, au kutia mapenzi baina ya wawili.

rejea, (Al Mughni 10/104)


Amesema Ibnu Qayyim; 
Sihri ni Mchanganyiko wa athari za mapepo wachafu na athari za nguvu ya kimaumbile.

rejea, (Zadul Ma`ad 4/126)



TAARIFU YA SIHIRI.

Sihiri ni maafikiano baina ya mchawi na shetani juu ya mchawi atende baadhi ya mambo ni haram au ya ushirikina katika mkabala wa shetani kumsaidia yeye na kumtii katika analolitaka.



kwa mukhtasari huo tujifunze;

▪Mume Anafungwa vipi asiweze kujamii,

▪Fiziolojia ya kujamii kwa mwanaume,

▪Fundo la Mwanamke Mume asiweze kumjamii,


KUFUNGWA KWA MWANAUME ASIWEZE KUMJAMII MKEWE.


▪Ni mwanamume aliye kamili kimaumbile na ambaye si mgonjwa, Anashindwa kumjamii mkewe.


Tunapotaka kujua mtu hufungwaje, hapana budi kwanza tujue namna ya dhakari inavyosimama.


FIZIOLOJIA YA KUJAMII KWA MWANAMUME:


👉🏿Dhakari ni kipande cha nyama kinachonyambulika, Damu ikisukumwa humo husimama, Na damu ikirejea,  nayo hulegea.


DHAKARI HUSIMAMA KUPITIA HATUA TATU:


1. Kichocheo cha kijinsia (kujamii) kinapotokeza kwa mwanamume, mapumbu huwa yakitoa homoni inayozimimina katika damu. Zile homoni hufika mpaka kichwani na hujaa mwili mzima kama vile mkondo wa umeme.

2. Kichocheo cha kijinsia hufika katika kituo chake makhsusi cha kazi hiyo katika ubongo.

3. Kituo cha kichocheo cha kijinsia katika ubongo, nacho hutuma ishara kwa haraka hadi katika kituo cha mishipa ya uzazi katika uti wa mgongo, ndipo vali ya mshipa wadamu iliyokuwa imefungwa, huanza kufunguka, damu ikaanza kububujika kwa nguvu katika viungo vya uzazi ikielekea katika dhakari ikimimina damu na hapo ika simama.


JINSI MWANAUME HUFUNGWA ASIWEZE KUMJAMII MWANAMKE:


Shetani Wa sihiri hukita katika ubongo wa mwanamume hasa katika kituo cha kichocheo cha kijinsia kinachotuma ishara hadi katika viungo vya uzazi, halafu huviacha viungo vya uzazi vikafanya kazi yake kama kawaida.

▪Wakati anapomkaribia mkewe na akataka kumjamii,  Shetani hukiharibu kituo cha kichocheo cha kijinsia katika ubongo, basi zikasimama ishara zote zinazotumwa katika viungo vinavyosukuma  damu katika uume ili usimame, Hapo ndipo damu inaporejea haraka kutoka katika uume ukaanza kulegea na kusinyaa.

▪Kwa ajili hiyo, utamuona mwanamume yu kawaida wakati anapochezacheza na mkewe - yaani uume wake umesimama wima lakini anapomkaribia kwa tendo la ndoa, husinyaa na asiweze kumjamii mkewe wa halali, kwa sababu uume kusimama, ndio jambo la msingi katika kukamilisha shughuli ya jimai kama tujuavyo.

▪Wakati mwingine utamkuta mtu ameowa wake wawili naye amefungwa kwa mmoja tu .  Kwa sababu shetani wa sihiri, hukiharibu kituo cha kichocheo cha kijinsia anapomkaribia, kwa sababu huyo shetani amepewa kazi ya kumfunga na huyo mmoja tu.


JINSI MWANAMKE HUFUNGWA KWA MUMEWE.


▪Kama Vile mwanamke hufungwa asiweze kumuingilia mkewe, vilevile mwanamke naye hufungwa kwa mumewe. 

Kufungwa kwa Mwanamke ni kwa aina tano:

1. FUNDO LA MWANAMKE:

▪Ni Mwanamke ajaribu kuzuwia mumewe kumjamii. Huwa akiyashikamanisha mapaja yake kwa namna ambayo mwanamume hawezi kumjamii. Hali hiyo ipo nje ya matakwa ya mwanamke. (Sio kupenda kwa mke mume asimjamii bali ni Sihiri ndiyo humfanya hivyo bila kutaka)



2. FUNDO LA UBUTU (wa kuhisi).

▪Jini aliyewakilishwa kwa sihiri, hufanya makazi katika kituo cha hisia katika ubongo wa mwanamke, mumewe anapotaka kumjamii, yule jini humkosesha hisia akawa hahisi ladha wala raha wala hampokei kwa mahaba mumewe, mbele yake huwa kama aliyefishwa ganzi, humfanya atakavyo (lakini hata habari hana). Tezi yake huwa haitoi kiowevu kinachorutubisha uchi wa mwanamke, hivyobasi shughuli ya jimai huwa haikamiliki kwa usanifu.


3. FUNDO LA KUTOKWA DAMU:


▪Aina hii ya sihiri huhitalifiana na sihiri ya kutokwa damu kwa jambo moja, nalo ni kuwa , fundo la kutokwa damu linahusu wakati wa kujamiiana tu, ama sihiri ya kutokwa damu, haina uhusiano na jambao hilo , bali huendelea siku nyingi.


Fundo la kutokwa damu ni mwanamume anapotaka kumjamii mkewe, shetani humsababishia kutokwa damu nyingi (istihadha), hapo mwanamume asiweze kumjamii.

kwa hali hiyo damu itamtoka kipindi chote upo nae ila ukiondoka au ukiwa haupo inakatika au unapotaka kumwingilia damu inaanza kutoka.


4. FUNDO LA KIZIBO:

▪Mwanamume anapotaka kumjamii mkewe, hupata kizuizi kigumu cha nyama asichoweza kukitoboa; Shughuli ya kukutana kijinsia isifaulu.


5. FUNDO LA KUONGEZA KINA CHA UKE


▪Mwanamume atamuowa msichana bikira, anapomjamii anamkuta kama mke mkuu kabisa hata anamshuku. Lakini anapotibiwa , Sihiri hubatilika na utando wa ubikira hurudi kama ulivyokuwa.


TAFAUTI BAINA YA FUNDO, KUTODISA (uume kutosimama) NA UDHAIFU WA NGUVU ZA KIUME.



▪KWANZA; FUNDO:

Aliyefungwa huhisi nishati na uwezo kamili wa kumjamii mkewe, bali uume husimama maadamu yu mbali naye, lakini anapomkaribia na akataka kumjamii, uume husinyaa na kutoweza kumjamii mkewe.

▪KUTODISA: (uume kutosimama).

Kutodisa maana yake ni mwanamume kutoweza tendo la kujamii, ima awe karibu au mbali na mkewe, bali uume hausimami aslan .


▪UDHAIFU WA NGUVU ZA KIUME:

Mwanamume huwa hawezi kumjamii mkewe ela katika nyakati mbalimbali, Na kumjamii kwenyewe humaliza katika muda mchache tu pamoja na uume kusinyaa baada ya kujimai.


JINSI YA KUTIBU SIHIRI YA MAFUNDO.

MKE AU MUME ALIYEFUNGWA ASIWEZE KUMUINGILIA MKEWE.

🍃Chukua majani saba mabichi ya mkunazi ya twange vizuri.






Yatie kwenye chombo chenye maji

Ukaribize mdomo karibu na maji huku ukiyakoroga majani katika maji naukisoma Ayatul Kursy na (Mu`awwidhati) 

mpe mgonjwa anywe na kuogea maji haya siku kadhaa  kwa uwezo wa Allahﷻ  Sihiri na Mafundo yatabatilika.


Rejea kitabu;

الصارم البتار فی التصدي للسحرة الأشرار












Mwandishi Abuu Ajmi حفظه الله 




_____________________________________


Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia


+255758200163

+254743101242


DAR ES SALAM

TANZANIA.






🔴TUWEWAADILIFU USIBADILI CHOCHOTE KWENYE MAKALA HII.


▪️▫️◾️◽️◼️◻️⬛️◻️◼️◽️◾️▫️▪️



CHANGO

CHANGO . watu wengi wanauliza chango ni nini ?  Chango ni jina la kiswahili lipatikanalo kwa baadhi ya makabila ya kibantu. Maana ya chango ...