UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO
Ugonjwa wa Vidonda vya tumbo (peptic ulcers ), au madonda yanayotokea katika tabaka la tumbo au kwenye duedenum (sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba ), huwa vikali sana na vinauma mno .
Kawaida maumivu na uchungu wa peptic ulcer hutambulika kama maumivu ya tumbo mara nyingine husababisha maumivu ya kifua .
SIFA ZA MAUMIVU.
Maumivu yanayo zalishwa na peptic ulcer yanatambulika kwa kuunguza (burning) au kuwaka moto .
Maumivu huzidi mara ulapo chakula au huzidi zaidi unapokula baadhi kama kunywa kahawa , pombe, kutafuna gums , kuvuta sigara .
Maumivu yanaweza kuambatana na Gesi tumboni , kichefuchefu, kutapika na kiungulia .
CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO . (PEPTIC ULCERS ).
Vidonda vya tumbo vinaweza kutokea wakati ute /kamasi au utelezi unaolinda sehemu ya juu ya utumbo imepungua au uzalishaji wa acidi tumboni kuongezeka .
Hali zinazo sababisha mara nyingi vidonda vya tumbo (peptic ulcers ) kwa watu wengi ni njia za usagaji wa chakula kutawaliwa na bakteria helicobacter pylori . Na pia matumizi ya NSAID (dawa) za kutuliza maumivu huzidisha uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo (peptic ulcers).
UHUSIANO KATI YA VIDONDA VYA TUMBO NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UGUMBA.
✍ Helicobacter Pylori (H. Pylori) ni bakteria ambaye hushambulia sehemu ya mwisho ya tumbo la chakula ( gastro ) na sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo ( duodenum ) ijulikanayo kama ( grastoduodenal tract ) na kupelekea tatizo la vidonda vya tumbo ( peptic ulcers ) na huyo bakteria watu humpata kupitia matumizi ya maji, vyakula na vyombo vyenye huyo bakteria kutokana na kutokusafishwa ipasavyo.
Maambukizi ya H pylori hayaishiitu katika sehemu ya mwisho ya utumbo mkubwa na sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo ( gastroduodenal tract ) bali husababisha mpaka magonjwa mengine ndani na nje ya mfumo wa chakula.
Kutokana na utafiti uliofanywa ulionesha H pylori anauwezo wa kusababisha magonjwa nje ya mfumo wa chakula kama magonjwa katika
➡Moyo
➡Mishipa ya damu
➡Kolomeo
➡Ngozi
➡Mfumo wa hewa
➡Mfumo wa homoni
➡Mfumo wa kinga ya mwili
➡Mfumo wa utengenezaji wa damu
➡Mfumo wa ubongo na utiwa wa mgongo.
Hivi karibuni ushahidi kutokana na utafiti umeonesha kuwepo ongezeko la tatizo la ugumba kwa wanaume na wanawake wenye H pylori zenye gene iitwayo CagA kulinganisha na wale ambao hawana H pylori
Kupitia njia mbali mbali H pylori mwenye gene CagA huweza kuchochea uzalishaji wa vichochezi vya inflammation na kinga za mwili ambazo huweza kuathiri moja kwa moja ama kwa njia nyingine mfumo wa uzazi.
Kwa wale watu wenye Vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na
H Pylori zenye gene ya CagA huweza kupelekea uharibifu wa mbegu za uzazi kwa wanaume na wananawake kwa kupunguza uwezo wa hizo mbegu kusafiri ( low motility), kuwa na nguvu na ustahimilivu (low vitality) ama uharibifu wa muonekano wa hizo mbegu
( Sperm cell morphology destruction )
Na huu uharibifu wa hizi H pylori haujajulikana unakuwaje bali inadhaniwa inaweza kuwa kwa njia mbili kwa upande wa wanaume;
A- kwa kuchochea kinga za mwili ambazo hushambulia kuta za seli ambazo huzalisha mbegu za kiume
B- kwa kuchochea mwili kuzalisha vichochezi ( inflammatory mediators ) kama interleukin na necrosis factor ambazo huenda na kushambulia mbegu za kiume.
Na kwa upande wau wanawake mapendekezo ni mengi ila inadhaniwa H pylori mwenye gene CagA huweza kuchochea uzalishaji wa kinga za mwili ambazo hupelekea mabadiliko katika mji wa uzazi ( uterus ) ambayo huathiri taratibu za Mbegu za kiume kuungana na yai la mwanamke.
Kutokana na tafiti hizo inaonesha vidonda vya tumbo husasababisha upungufu wa nguvu za kiume na uwezo wa mwanamke kupata mimba.
Ni dhahiri kwa wanaosumbuliwa na vidonda vya tumbo huweza kupungukiwa nguvu za kijinsia na kupelekea;
1. kukosa hamu ya tendo la ndoa
2. Kushindwa kufanya tendo la ndoa
( kwa wanaume )
3. Uume kuwa legelege kutokana na athari za vidonda vyatumbo
( kwa wanaume )
4. kushindwa kushika au kutungisha mimba
Hivyo basi kwa wale wenye vidonda vya tumbo ni vyema kutibu chanzo hiki kabla ya matumizi ya dawa za uzazi.
Tumia Shifaa Dawa ya vidonda vya tumbo.
VITU VYA KUEPUKA KWA MWENYE VIDONDA VYA TUMBO
🔥Epuka Chumvi nyingi kwenye mlo
🔥Epuka Mafuta mengi kwenye mlo
🔥Epuka kula Nyama nyekundu (Ng`ombe, Mbuzi , Kondoo n.k)
🔥Epuka matumizi ya Tangawizi , pilipili manga
🔥Epuka kula Nanasi ,Fenesi
🔥Epuka kunywa Maziwa
🔥Epuka kula Machungwa , Limao ndimu
🔥Epuka kula Maharage na vyakula vyote unapokula tumbo linajaa gesi viepuke .
🔥Epuka Kutafuna gum, (Big G bablish,ballgum, pk n.k)
🔥Epuka ugali wa sembe)
________________________
VITU VYA KUACHA KABISA
❌Acha kunywa Pombe
❌Acha Kunywa Soda (Carbonated beverages).
❌Acha kuvuta Sigara
❌Acha kula miraa
MWANDISHI ....✍ ABUU NAWFAL MZAMIRU KATUNZI NA ABUU AJMI
Rejea;-
1. World Journal of Gastroenterology.
8226 Regency drive ,Pleasanto, CA 94588, USA ©2014
2. Wei Wu1, Qiuqin Tang2, Hao Gu1, Yiqiu Chen1, Yankai Xia1, Jiahao Sha3 and Xinru Wang1 Address all correspondence to: wwu@njmu.edu.cn; xrwang@njmu.edu.cn
1 State Key Laboratory of Reproductive Medicine, Department of Toxicology, School of Public Health, Nanjing Medical University, Nanjing, China
2 State Key Laboratory of Reproductive Medicine, Department of Obstetrics, Nanjing Maternity and Child Health Care Hospital Affiliated to Nanjing Medical University, Nanjing, China
3 State Key Laboratory of Reproductive Medicine, Nanjing Medical University, Nanjing, China
WASILIANA NASI KWA DAWA NZURI YA VIDONDA VYA TUMBO NA NGUVU ZA KIUME.
________________________________
Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia
+255758200163
+254743101242
DAR ES SALAM
TANZANIA.
jiunge chanel yetu kwa masomo mbalimbali ya tiba Asilia
No comments:
Post a Comment