Wednesday, June 3, 2020

SIHIRI /UCHAWI /KIJICHO.

SIHIRI/UCHAWI AU KIJICHO.
                



Amesema Ibnu Qudama Al Maqdisy; 
Sihiri(uchawi) ni kifundo, zunguo na maneno yanayosemwa au kuandikwa, au afanye jambo litakaloathiri katika mwili wa aliyesihiriwa au moyoni mwake au akilini mwake bila  ya kumshika.  Nayo ina uhakika, Kuna yenye  kuuwa, yenye kutia maradhi, inayomzuia mwanaume asiweze kumjamii mkewe. Muna na inayomtenganisha mtu na mkewe na inayomchukiza mmojawapo kwa mwenzie, au kutia mapenzi baina ya wawili.

rejea, (Al Mughni 10/104)


Amesema Ibnu Qayyim; 
Sihri ni Mchanganyiko wa athari za mapepo wachafu na athari za nguvu ya kimaumbile.

rejea, (Zadul Ma`ad 4/126)



TAARIFU YA SIHIRI.

Sihiri ni maafikiano baina ya mchawi na shetani juu ya mchawi atende baadhi ya mambo ni haram au ya ushirikina katika mkabala wa shetani kumsaidia yeye na kumtii katika analolitaka.



kwa mukhtasari huo tujifunze;

▪Mume Anafungwa vipi asiweze kujamii,

▪Fiziolojia ya kujamii kwa mwanaume,

▪Fundo la Mwanamke Mume asiweze kumjamii,


KUFUNGWA KWA MWANAUME ASIWEZE KUMJAMII MKEWE.


▪Ni mwanamume aliye kamili kimaumbile na ambaye si mgonjwa, Anashindwa kumjamii mkewe.


Tunapotaka kujua mtu hufungwaje, hapana budi kwanza tujue namna ya dhakari inavyosimama.


FIZIOLOJIA YA KUJAMII KWA MWANAMUME:


👉🏿Dhakari ni kipande cha nyama kinachonyambulika, Damu ikisukumwa humo husimama, Na damu ikirejea,  nayo hulegea.


DHAKARI HUSIMAMA KUPITIA HATUA TATU:


1. Kichocheo cha kijinsia (kujamii) kinapotokeza kwa mwanamume, mapumbu huwa yakitoa homoni inayozimimina katika damu. Zile homoni hufika mpaka kichwani na hujaa mwili mzima kama vile mkondo wa umeme.

2. Kichocheo cha kijinsia hufika katika kituo chake makhsusi cha kazi hiyo katika ubongo.

3. Kituo cha kichocheo cha kijinsia katika ubongo, nacho hutuma ishara kwa haraka hadi katika kituo cha mishipa ya uzazi katika uti wa mgongo, ndipo vali ya mshipa wadamu iliyokuwa imefungwa, huanza kufunguka, damu ikaanza kububujika kwa nguvu katika viungo vya uzazi ikielekea katika dhakari ikimimina damu na hapo ika simama.


JINSI MWANAUME HUFUNGWA ASIWEZE KUMJAMII MWANAMKE:


Shetani Wa sihiri hukita katika ubongo wa mwanamume hasa katika kituo cha kichocheo cha kijinsia kinachotuma ishara hadi katika viungo vya uzazi, halafu huviacha viungo vya uzazi vikafanya kazi yake kama kawaida.

▪Wakati anapomkaribia mkewe na akataka kumjamii,  Shetani hukiharibu kituo cha kichocheo cha kijinsia katika ubongo, basi zikasimama ishara zote zinazotumwa katika viungo vinavyosukuma  damu katika uume ili usimame, Hapo ndipo damu inaporejea haraka kutoka katika uume ukaanza kulegea na kusinyaa.

▪Kwa ajili hiyo, utamuona mwanamume yu kawaida wakati anapochezacheza na mkewe - yaani uume wake umesimama wima lakini anapomkaribia kwa tendo la ndoa, husinyaa na asiweze kumjamii mkewe wa halali, kwa sababu uume kusimama, ndio jambo la msingi katika kukamilisha shughuli ya jimai kama tujuavyo.

▪Wakati mwingine utamkuta mtu ameowa wake wawili naye amefungwa kwa mmoja tu .  Kwa sababu shetani wa sihiri, hukiharibu kituo cha kichocheo cha kijinsia anapomkaribia, kwa sababu huyo shetani amepewa kazi ya kumfunga na huyo mmoja tu.


JINSI MWANAMKE HUFUNGWA KWA MUMEWE.


▪Kama Vile mwanamke hufungwa asiweze kumuingilia mkewe, vilevile mwanamke naye hufungwa kwa mumewe. 

Kufungwa kwa Mwanamke ni kwa aina tano:

1. FUNDO LA MWANAMKE:

▪Ni Mwanamke ajaribu kuzuwia mumewe kumjamii. Huwa akiyashikamanisha mapaja yake kwa namna ambayo mwanamume hawezi kumjamii. Hali hiyo ipo nje ya matakwa ya mwanamke. (Sio kupenda kwa mke mume asimjamii bali ni Sihiri ndiyo humfanya hivyo bila kutaka)



2. FUNDO LA UBUTU (wa kuhisi).

▪Jini aliyewakilishwa kwa sihiri, hufanya makazi katika kituo cha hisia katika ubongo wa mwanamke, mumewe anapotaka kumjamii, yule jini humkosesha hisia akawa hahisi ladha wala raha wala hampokei kwa mahaba mumewe, mbele yake huwa kama aliyefishwa ganzi, humfanya atakavyo (lakini hata habari hana). Tezi yake huwa haitoi kiowevu kinachorutubisha uchi wa mwanamke, hivyobasi shughuli ya jimai huwa haikamiliki kwa usanifu.


3. FUNDO LA KUTOKWA DAMU:


▪Aina hii ya sihiri huhitalifiana na sihiri ya kutokwa damu kwa jambo moja, nalo ni kuwa , fundo la kutokwa damu linahusu wakati wa kujamiiana tu, ama sihiri ya kutokwa damu, haina uhusiano na jambao hilo , bali huendelea siku nyingi.


Fundo la kutokwa damu ni mwanamume anapotaka kumjamii mkewe, shetani humsababishia kutokwa damu nyingi (istihadha), hapo mwanamume asiweze kumjamii.

kwa hali hiyo damu itamtoka kipindi chote upo nae ila ukiondoka au ukiwa haupo inakatika au unapotaka kumwingilia damu inaanza kutoka.


4. FUNDO LA KIZIBO:

▪Mwanamume anapotaka kumjamii mkewe, hupata kizuizi kigumu cha nyama asichoweza kukitoboa; Shughuli ya kukutana kijinsia isifaulu.


5. FUNDO LA KUONGEZA KINA CHA UKE


▪Mwanamume atamuowa msichana bikira, anapomjamii anamkuta kama mke mkuu kabisa hata anamshuku. Lakini anapotibiwa , Sihiri hubatilika na utando wa ubikira hurudi kama ulivyokuwa.


TAFAUTI BAINA YA FUNDO, KUTODISA (uume kutosimama) NA UDHAIFU WA NGUVU ZA KIUME.



▪KWANZA; FUNDO:

Aliyefungwa huhisi nishati na uwezo kamili wa kumjamii mkewe, bali uume husimama maadamu yu mbali naye, lakini anapomkaribia na akataka kumjamii, uume husinyaa na kutoweza kumjamii mkewe.

▪KUTODISA: (uume kutosimama).

Kutodisa maana yake ni mwanamume kutoweza tendo la kujamii, ima awe karibu au mbali na mkewe, bali uume hausimami aslan .


▪UDHAIFU WA NGUVU ZA KIUME:

Mwanamume huwa hawezi kumjamii mkewe ela katika nyakati mbalimbali, Na kumjamii kwenyewe humaliza katika muda mchache tu pamoja na uume kusinyaa baada ya kujimai.


JINSI YA KUTIBU SIHIRI YA MAFUNDO.

MKE AU MUME ALIYEFUNGWA ASIWEZE KUMUINGILIA MKEWE.

🍃Chukua majani saba mabichi ya mkunazi ya twange vizuri.






Yatie kwenye chombo chenye maji

Ukaribize mdomo karibu na maji huku ukiyakoroga majani katika maji naukisoma Ayatul Kursy na (Mu`awwidhati) 

mpe mgonjwa anywe na kuogea maji haya siku kadhaa  kwa uwezo wa Allahﷻ  Sihiri na Mafundo yatabatilika.


Rejea kitabu;

الصارم البتار فی التصدي للسحرة الأشرار












Mwandishi Abuu Ajmi حفظه الله 




_____________________________________


Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia


+255758200163

+254743101242


DAR ES SALAM

TANZANIA.






🔴TUWEWAADILIFU USIBADILI CHOCHOTE KWENYE MAKALA HII.


▪️▫️◾️◽️◼️◻️⬛️◻️◼️◽️◾️▫️▪️



No comments:

CHANGO

CHANGO . watu wengi wanauliza chango ni nini ?  Chango ni jina la kiswahili lipatikanalo kwa baadhi ya makabila ya kibantu. Maana ya chango ...