FUNGASI NI NINI ?
MWANDIAHI; DR. ABUU ABAYDULLAH حفظه الله
✍🏽Mapunye ni ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na fungus jamii ya Tinea.
👉🏽Jamii hizi za fungus hupewa majina kutokana na sehemu ya ngozi inayoshambulia
Mathalani pindi zinaposhambulia;
◼-Kichwani yaitwa Tinea capitis
◼-Mwilini naitwa Tinea corporis
-Sehemu za siri yaitwaTinea pubis
◼-Katikati ya vidole vya miguu yaitwa Tinea ungium.
💢Muonekano wake;
🔴Za kichwani na mwilini huwa zinakaribia kuwa sawa, huwa zinaanza kuwa na mduara uliotengenezwa na vijipele vyekundu .
Vya katikati ya vidole huwa ni utando mweupe ulio katikati ya vidole( mara nyingi kutokea kwenye vidole vya mwisho ambavyo vimeshikana kiasi cha kukosa nafasi)
DALILI ZA FUNGUS ZA MWILINI (TINEA)
🔴Tinea capitis na corporis na pubis :
👉🏽uwepo wa mapunye +/- muwasho wa sehemu husika ,
👉🏽kutoa maji maji sehemu husika au kutunga usaha( hapo itaashiria na uwepo wamashambulizi ya baccteria)
Tinea ungium; huwa ni uwepo wa huo utando+/- muwasho wa sehemu husika na harufu mbaya katikati ya vidole.
MATIBABU YA HOSPITALI
👉🏽tunatoa topical anti fungals kama Whitefield cream( huwa inakawaida ya kuwasha ila ni nzuri) na miconazole cream. Pia na ant biotics kama mupurocin cream kama kutakuwa na bacteria infection.
USHAURI/JINSI YA KUJIKINGA
💧Jitahidi suala la usafi yaani kuoga angalau mara 2 kwa siku na sabuni( kwa fungus za mwilini na kichwa),
Kujitahidi kukausha majimaji yanayobakia katikati ya vidole.
✍🏽NYONGEZA KUTOKA KWA DR. ABUU HUDHAIFAH حفظه الله
Kwa kuongezea katika maelezo ya daktari hapo juu ni kwamba fungus ni kitu nyemelezi na vinapopatikana mazingira rafiki basi hujitokeza;
🍀1.kinga ya mwili kuwa chini mfano kwa kisukari,saratani, virusi vya ukimwi,matumizi makubwa ya dawa aina za steroid na antibiotic ,
🍀2.Mazingira ya unyevu unyevunyevu,
🍀3.Kutokutumia dawa za fangus kwa kipindi kinachotakiwa ,
🍀4.kutokufata maelekezo ya namna ya kutibu sababu ya awali primary cause.
BARAKAALLAHU FIYKUM
DAWA ASILIA ZA FUNGUS ZA MIGUU.
Unga wa majani ya mpera changanya na maji kidogo . Paka katikati ya vidole vilivyo na fungasi (twanga unga uwe laini sana ).
2⃣KITUNGUU SAUMU NA MAFUTA YA ZAITUN .
Twanga vitunguu saumu kisha vitie katika maji vuguvugu loweka miguu nusu saa .
👉Twanga vitunguu saumu viwe rojo laini changanya na mafuta ya zaytuni ujazo sawa .
pakaa katika katika ya vidole x3 kwa siku .
👉Tafuna punje 3 za vitunguu saumu asubuhi kabla hujala chohote na tia vitunguu saumu katika mapishi ya mlo wako.
DAWA NA ABUU AJMI حفظه الله
_______________________________
Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia
+255758200163
+254743101242
DAR ES SALAM
TANZANIA.
🔴TUWEWAADILIFU USIBADILI CHOCHOTE KWENYE MAKALA HII.
▪️▫️◾️◽️◼️◻️⬛️◻️◼️◽️◾️▫️▪️
No comments:
Post a Comment