Wednesday, June 10, 2020

PTOSIS

UGONJWA PTOSIS
_______________________


Ptosis ni hali hutokea kigubiko cha juu cha jicho au macho yote hushuka.

Ushukaji unaweza kuwa mdogo usiodhirika mpaka atizame kwa kiyoo au unaweza kuwa mkubwa anao uhisi sana au  kuwa mkubwa hata kuzui kuona.



Kushuka kwa kigubiko cha jicho hutokea kwa sababu misuli ya levator (misuli inahusika na kunyanyua na kushusha kigubiko cha jicho) Imeadhirika.


ZIPO AINA SITA ZA PTOSIS.
_________________________


1. APONEUROTIC PTOSIS. 

Hii ndiyo hali maarufu zaidi ambayo inahusishwa na kuzeeka.

Misuli ya levator inakuwa imetumika sana na haina uwezo wa kujirudisha kama ilivyofanya awali.

Hali hii inaweza sababishwa na kupikicha jicho sana au matumizi ya lensi muda mrefu.

2. NEUROGENIC PTOSIS.


Hali hii hutokea njia za  nerves zinazo dhibiti harakati za kigubiko cha jicho zimeharibika.

hali hii inaweza sababishwa na Horner syndrome, third nerve palsy, au myasthenia gravis.


3. MYOGENIC PTOSIS.

Hali hii hutokea maradhi yanayo athiri mifumo ya mwili kama mafua na shinikozo la damu,Kisukari husababisha udhaifu wa misuli kama udhaifu wa mshikamano wa misuli.

Hali hii huchangia pia kutokana na misuli mingine mwilini kuendelea kudhofika, wakati mwingine hata misuli ya levetor.




4. MECHANICAL PTOSIS.

Kama kigubiko cha jicho kimelemewa na mkandamizo uliozidi wa ngozi Mechanical ptosis inaweza kutokea.

5. TRAUMATIC PTOSIS

Ptosis inaweza kutokana na majeraha au maumivu ya ndani ya kigubiko cha jicho au jicho .

Hali hii hutokana na kutokuvaa vizuizi vya macho wakati wa kazi zinazohitajia hivyo kama uchomeleaji au baadhi ya michezo inayo inayohitaji kuvaa vizuizi.

6. CONGENITAL PTOSIS.

Watoto wanaweza kuzaliwa na kigubiko cha jicho kilichoshuka.

Hali hii hutokea misuli ya levetor haijakuwa vizuri katika fuko la uzazi.

Imtokeapo mtoto hali hii inabidi afanyiwe vipimo na tiba ya haraka. Kadri mtoto anavyokuwa hali hii inazidi kuwa mbaya.

No comments:

CHANGO

CHANGO . watu wengi wanauliza chango ni nini ?  Chango ni jina la kiswahili lipatikanalo kwa baadhi ya makabila ya kibantu. Maana ya chango ...