Monday, June 8, 2020

HUKMU YA KUPANDIKIZA MIMBA .


اَلسَلامُ عَلَيْكُم وَرَحْمَةُ اَللهِ وَبَرَكاتُهُ‎‎


Afwan mwalimu wetu mbora , Tunaomba tusaidie kuhusu jambo hili la kupandikiza mimba katika kizazi je mwalimu wetu mbora inafaa kufanya hivyo ?


kama inafaa zipi sharti  zake?

BarakaAllahu fiyka .

JAWABU ;
Sheikh Abū Ayman bin Akida Dhahiir Al-Shiiraaziy Al-Shāfi'iyy حفظه الله

 وعليكم السلام ورحمة الله وبركاته

 Jambo hili ni jambo la khatari sana kama walivyosema 'Ulamaa, na limekaliwa na tume ya Fiqh kule Makkah, wakatoa tija ambayo naifupisha ifuatavyo

Kama mke wamethibitisha Madaktari wahusika kuwa ni tasa basi haifai kufanya hiyo amaliyyah.


Kama mke si tasa ila ana hitlafu fulani inayosababisha kutokufika manii ya mumewe mahala panapostahiki basi amaliyyah hiyo itafaa kwa sharti mume mwenyewe ndo amkabidhi Dr wa kike manii yake ili amuwekee mwanamke mahala husika, akikosekana Dr wa kike basi mwanaume atakuwa ni nambari mbili kwa maana baada ya kukoseKana nambari moja ambaye ni wakike. 

Na hiyo amaliyyah ifanyike wakiwepo watu watatu tu, mume lazima ashuhudie, mke mfanyiwa amaliyyah  hiyo pamoja na Dr atakayemuweka hizo mbegu.

Pamoja ya ruhusa hiyo ila bado wanasema 'Ulamaa awla ni kuacha kufanya hivyo japo hawajaharamisha.

Nimetohoa hayo kutoka katika fat'wa ya 'Allāmah bin Baaz (Allāh amrahamu).



JAWABU;  Sheikh Abū Ayman bin Akida Dhahiir Al-Shiiraaziy Al-Shāfi'iyy حفظه الله






Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia

+255758200163
+254743101242

DAR ES SALAM
TANZANIA.





No comments:

CHANGO

CHANGO . watu wengi wanauliza chango ni nini ?  Chango ni jina la kiswahili lipatikanalo kwa baadhi ya makabila ya kibantu. Maana ya chango ...