Maambukizi ya bacteria huweza kuathiri sehemu yoyote ya mfumo huu. Maambukizi ya mfumo wa mkojo ni ya pili ukiangalia maambukizi yote ya mwili.
DALILI ZA MAAMBUKIZI YA MFUMO WA MKOJO.
Dalili hutofautiana kulingana na ukali wa maambukizi,umri na sehemu iliyoathirika.
Dalili zinazojitokeza mara nyingi pakiwa na maambukizi (UTI):
▶Uchungu au kuwashwa unapokojoa.
▶Kuhisi kukojoa mara nyingi.
▶Homa na uchovu .
▶Mkojo wenye harufu mbaya na si safi (cloudy).
DALILI ZINAZOTOKANA NA MAAMBUKIZI YA KIBOFU CHA MKOJO.
▶Maumivu katika upande wa chini wa tumbo.
▶Kukojoa mkojo kidogo , wenye maumivu na mara nyingi.
▶Dalili za homa kidogo. Bila maumivu ya mbavu.
▶Damu kwenye mkojo.
DALILI ZINAZOTOKANA NA MAAMBUKIZI YA UPANDE WA JUU WA NJIA YA MKOJO.
▶Maumivu ya upande wa juu wa mgongo na mbavu.
▶Kuwa na homa na kuhisi kibaridi. Kichefuchefu, kutapika, uchovu na kujihisi mgonjwa kwa ujumla.
▶Kuchanganyikiwa kwa wazee.
🔥Maambukizi haya ni hatari sana yasipotibiwa vyema na haraka. Aidha yanaweza hata kuhatarisha maisha.
Kuwashwa na kukojoa mara nyingi ni dalili za maambukizi ya sehemu za mfumo wa mkojo.
CHANZO CHA MAAMBUKIZI YA MARA KWA MARA YA NJIA YA MKOJO.
➡Kuziba kwa njia ya mkojo.
➡Maumbile ya kike Kwa sababu njia ya yurethra ya wanawake ni fupi kuliko ya wanaume,basi huwezekano wa kupata maambukizi ni mkubwa zaidi kuliko wanaume.
➡Maingiliano/ Kujamiiana: Wanawake wanaoshiriki tendo la ndoa huweza kupata maambukizi mengi zaidi kuliko wenzao wasioshiriki tendo hilo.
➡Mawe Mawe kwenye figo, njia ya kuelekea kwenye kibofu cha mkojo (ureta) au ndani ya kibofu chenyewe yanaweza kuzuia mtiririko wa mkojo na hivyo kusababisha maambukizi.
➡Mpira wa katheta Watu waliowekewa katheta wana uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi kirahisi.
➡Kasoro za kimaumbile Watoto wenye kasoro za kimaumbile kama mkojo kurudi nyuma kama kwenye kibofu na hivyo kwenda kwenye yureta ( vesicoureteral reflux) au kama njia ya yurethra valve inafungukia nyuma, hupata maambukizi kwa urahisi sana.
➡Kuongezeka ukubwa wa tezi dume Wanaume walio na umri wa miaka zaidi ya sitini wanaweza kupata maambukizi kwa sababu ya kukua kwa tezi dume.
➡Kinga ya mwili iliyodhoofika Wagonjwa wa kisukari,UKIMWI au saratani.
➡Sababu nyingine: kama njia za yureta na yurethra kuwa nyembamba,tibi (TB) kwenye njia ya mkojo, neurogenic bladder,diverticulum nk.
_______________________________
Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia
+255758200163
+254743101242
DAR ES SALAM
TANZANIA.
TUWEWAADILIFU USIBADILI CHOCHOTE KWENYE MAKALA HII.
No comments:
Post a Comment