DALILI ZA BAWASIRI ZINATEGEMEA NA AINA YA BAWASIRI.
1⃣BAWASIRI YA NJE.
Hutokeza nje ya ngozi inayozunguka dubri .
⭕Kuwashwa au kuwasha eneo linalozunguka dubri,
⭕Maumivu yenye kukera na kusumbua,
⭕Kiuvimbe kilicho tuna nje ya dubri,
⭕Kuvuja damu ,
- 2⃣BAWASIRI YA NDANI .
Bawasiri ya ndani ya utumbo wa mwisho karibu na dubri. Huwezi kuiona au kuihisi na mara chache husababisha usumbufu. Lakini kukaza au kuwasha wakati wa kupitisha haja kubwa kunaweza kusababisha ;
⭕Damu kutoka bila maumivu wakati wa kukidhi haja kubwa . Unaweza kuino kwenye choo au karatasi ya kujifutia (Tissue paper )
⭕Bawasiri (kinyama ) kutokeza kwenye dubri na kusababisha kuwashwa na maumivu.
3⃣Thrombosed hemorrhoids.
Kama damu itatuama katika bawasiri ya nje na kuganda (thrombus ), itasababisha-;
⭕Maumivu makali ,
⭕Kufura ,
⭕Uvimbemchungu wenye kuwasha ,
⭕Kivimbe kigumu kwenye dubri.
VISABABISHI VYA BAWASIRI.
Mishipa karibu na dubri huwa inajinyoosha kwa nguvu na kupanuka au kuvimba. Bawasiri inaweza kukua kutokana na shinikizo kubwa kwenye mfereji wa chini kutokana na -;
🔹Kujikaza wakati wa haja kubwa ,
🔹Kukaa muda mrefu wakati wa haja kubwa ,
🔹Kuharisha sana au kupata choo kwa tabu kama cha mbuzi,
🔹Ujauzito ,
🔹Kufanywa liwati kuingiliwa tundu la haja kubwa dubri,
🔹Kuinua mara kwa mara vitu vizito(sana ),
🔹Kunenepa sana,
🔹Ulaji wa vyakula visivyokuwa na kamba kamba/nyuzi (fibre).
Kadiri unavyozeeka, hatari ya kupata bawasiri inaongezeka .Kwa sababu tissue zinazo shikiza mishipa kwenye mreji na dubri zinaweza kuchoka na kulegea .
Hii inaweza tokea kwa mjazito , kwa sababu uzito wa mtoto hukandamiza eneo lote la dubri.
JINSI YA KUJIKINGA NA BAWASIRI .
🍀Kula vyakula vyenye nyuzi nyingi kama makoma ,
🍀Kunywa maji yakutosha,
🍀Usijikaze sana wakati wa haja kubwa,
🍀Jisadie haraka pindi unapohisi haja kubwa , ukichelewa kutoa kinyesi kinarudi na hisia hupotea , Choo kitakuwa kikavu na kigumu hata kushindwa kukitoa kutoka ,
🍀Fanya mazoezi ,
🍀Epuka kukaa chini sana . kukaa muda mrefu , haswa chooni kunaweza zidisha msukumo mkubwa wa mishipa kwenye dubri .
No comments:
Post a Comment