Saturday, June 13, 2020

TATIZO LA KUFA GANZI NA KICHWA KUUMA

KICHWA KUUMA NA KUFA GANZI


SWALI

Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakaat

Naomba ushauri ikitokea kuumwa kichwa tena huwa kama ganzi inaweza kuwa nini hapo.


JAWABU

📛Kichwa kuuma ni dalili ya maradhi mengi sana nani pamoja na hilo la pressure na shida ya macho pia

Miongoni mwa sababu za maumivu ya kichwa

♦️1.maambukizi mwilini mfano malaria,typhoid,maambukizi njia ya hewa n.k

♦️2.damu kuwa nyingi sana au kidogo sana

♦️3.shinikizo la damu

♦️4.presha kuwa chini

♦️5.matatizo ya macho ima ni eye defects au ongezeko la pressure ya macho

♦️6.kuwa na historia ya ajali sehem ya kichwa

♦️7.saratani ya ubongo na nyinginezo

♦️9.maradhi ya figo&inni

♦️10.kutokupumzika ipasavyo (tensions headache)

♦️11.kuwa na uraibu ama dependency ya dawa au vinywaji mfano soda,energy drinks,chai na kahawa

♦️12.msongo wa mawazo
N.k



SWALI LA NYONGEZA

Afwan Dr. hapo katika maelezo yake kuna hali ametaja kufa ganzi kichwa

hii haswa inaashiria nini haswa au nini sababu.

kutakuwa na sababu tofauti ya kufa ganzi au ni pamoja na hayo uliyo eleza?

pia zipo kadhia Dr. mtu amelala kisha kichwa kufa ganzi bila kuuma hii inatokana na nini Dr. Allah akuhifadhi.

JAWABU

🟢Baadhi niliyoyataja hapo juu hupelekea kichwa kufa ganzi kwa baadhi ya watu.

♦️Lakini pia ulalaji mbaya(poor sleeping posture) inaweza sababisha

👉Mfano mtu analalia kifua kwa muda mrefu ni dhahiri kwamba misuli ya shingo yake haiwi katika hali ya utulivu (relax) itakua ni yenye kujivuta upande mmoja zaidi ikitokeze mishipa ya upande mmoja haipeleki damu sawasawa kama inavyo takiwa basi mtu anaweza pata chamgamoto hiyo ya ganzi na misuli ya shingo kuwa na maumivu
Lakini si kila anaepata ganzi basi alilala vibaya laa!


Suluhu ni kuzishulikia sababu na si matokeo pekee kwa maana ukawa ni mtu wa kula dawa za maumivu kila siku


..✍ MTOA MAJAWABU
DR. ABUU HUDHAIFAH حفظه الله



Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia

+255758200163

+254743101242

DAR ES SALAM
TANZANIA.



🔴TUWEWAADILIFU USIBADILI CHOCHOTE KWENYE MAKALA HII.

▪️▫️◾️◽️◼️◻️⬛️◻️◼️◽️◾️▫️▪️

No comments:

CHANGO

CHANGO . watu wengi wanauliza chango ni nini ?  Chango ni jina la kiswahili lipatikanalo kwa baadhi ya makabila ya kibantu. Maana ya chango ...