UPUNGUFU WA TESTOSTERONE (MALE HYAPOGONADISM )
Male hypogonadism au upungufu wa testosterone (testosterone deficiency) hutokana na pumbu kushindwa kuzalisha homoni ya kijinsia ya kiume testosterone, manii au vyote.
Upungufu wa testosterone unaweza kutokana na maradhi ya pumbu au hali inayo adhiri hypothalamus au pituitary glands.
Hypogonadism inaweza athiri viungo vingine utendaji wake na kuvidhofisha visiweze kufanya kazi ipasavyo.
Testosterone , ni homoni ya kijinsia ya mwanaume inayotengenzwa katika pumbu .
Kuwa na kiwango cha kutosha cha testosterone ni muhimu kwa ukuaji wa kawaida wa kijinsia wa kiume na utendaji.
Testosterone zinamsaidia mvulana kukuza au kuwa na maumbile ya kiume kama kuota ndevu , nywele za sehemu za siri na makwapa , sauti nzito , kuongezeka nguvu ya misuli, kurefuka na kunenepa uume na pumbu kuongezeka wakati wa balekhe na pia inasaidia uzalishaji wa seli nyekundu za damu .
Wanaume wanahitaji testosterone kutengeneza manii (sperm) na seli nyekundu za damu .
Kiwango cha testosterone hupungua kadiri umri wa mtu unavyo ongezeka (uzee ).
Baadhi ya wanaume wana kiwango kidogo cha testosterone (Testosterone deficiency syndrome TD au Low Testosterone Low -T)
(DEFICIENCY) Upungufu wa testosterone , Inamaanisha mwili hauna kiwango cha kutosh kinachohitajika.
(Syndrome) Mjumuiko wa dalili ambazo kwa ujumla zinaashiria maradhi au hali ya kiafya .
Tatizo la upungufu wa testosterone homoni (Testosterone deficiencies sydrome) linatambulika kwa majina mengine kama;
🔸Male hypogonadism
🔸Testosterone deficiency,
🔸Primary hypogonadism,
🔸Secondary hypogonadism, 🔸Hypergonadotrophic hypogonadism,
🔸Hypogonadotrophic hypogonadism.
Wanaume wanaweza kuadhirika na upungufu wa testosterone katika umri wowote tangu kubalekhe kwa kutofautiana dalili na adhari.
DALILI ZA UPUNGUFU WA TESTOSTERONE (MALE HYPOGONADISM)
Dalili na ishara zinategemea na ukomavu wa kijinsia na rika lamgonjwa .
DALILI ZA UPUNGUFU WA TESTOSTERONE KABLA AU WAKATI WA KUBALEHE
Kama upungufu wa testosterone kabla au wakati wa kubalehe dalili zitakuwa kama hizi
▶Kuchelewa kubalekhe,
▶Pumbu na Uume kudumaa (kutoongezeka ukubwa)
▶Uhaba au kutoota ndevu na nywele seheme za siri
▶Sauti kutobadilika au kuwa na sauti laini ya kike.
▶Upungufu au pumbu kutozalisha manii na kusababisha ugumba
▶Mafupa kuchelewa kupevuka kulingani na umri (Kipindi cha balehe , mvulana mwenye testosterone chache hutokea muda mwingine akawa dhaifu wa mwili na mikono na miguu kukua bila uwiyano na mwili wake (kurefuka mikono na miguu zaidi ya umbile la mwili au kuwa mifupi).
DALILI ZA UPUNGUFU WA TESTOSTERONE KWA MWANAUME ALIYEFIKIA UKOMAVU WA KIJINSIA.
▶Kukosa hamu ya tendo la ndoa na uume kuwa legelege na kushindwa kufanya tendo la ndoa kikamilifu,
▶Kuchoka sana,
▶Kukosa uzingativu na ari,
▶Ndevu na nywele za sehemu za siri kutoota au kuwa chache,
▶Kupungua ujazo wa manii,
▶Pumbu kuwa laini sana na ndogo,
▶Kubadilika mihemko,
▶Kuongezeka mafuta mwilini,
▶Chuchu kutuna kama za binti (gynaecomastia),
▶Mifupa kuwa laini na mepesi hupelekea kuvunjika kirahisi (osteoporosis),
▶Kupungua misuli kujazia na nguvu ya mwili kuwa ndog,
▶Ngozi na uso kukunjana,
▶Kutoa jasho sana.
kwa dalili kama kuchoka mihemko kubadilika vinaweza kuwa na visababishi vingine tofauti tofaut.
MADHARA YA TESTOSTERONE KUWA NYINGI KWA MWANAUME.
Kiwango cha testosterone kinapokuwa kingi mwilini kinamadhara kwa wanaume kubalehe mapema chini ya miaka 9.
Kuzidi kwa testosterone kwa watu waliokwisha balehe hakuna madhara .
Kwa wanawake testosterone kuwanyingi kunasababisha madhara kama;
▶Kuvurugika mzunguko wa hedhi ,
▶Upara ,
▶Souti nzito,
▶Ukuaji na uvimbe wa clitoris,
▶Umbo kuwa kama mwanaume,
▶Matiti kuwa madogo sana,
▶Ngozi kuwa na mafuta mengi,
▶Chunusi,
▶Kuota ndevu na masharubu,
▶Kusabisha uvimbe kwenye kizazi.
VISABABISHI VYA TESTOSTERONE KUWA NYINGI KWA WANAWAKE .
Moja ya sababu ya wanawake kuwa na kiwango kingi cha testosterone ni kufanya mazoezi mazito , maradhi au mabadiliko ya homoni,
Sababu kuu za testosterone kuwanyingi kwa wanawake ni ; hirsutism, polycystic ovary syndrome, na congenital adrenal hyperplasia.
1. Hirsutism
Hirsutism, ni hali ya homoni inayosababisha ukuwaji wa nywele zisizohitajika kwa mwanamke kama mgongoni , kifuani . Kiwango cha nywele hutegemea sababu za kurithi ila kwa hali hii husababishwa na androgen homoni kutowiyana.
2. Polycystic ovary syndrome
Polycystic ovary syndrome (PCOS), hili ni tatizo lingine la homoni lisababishwalo na kiwango kikubwa cha androgen hormones kwa wanawake.
Kama mwanamke ana PCOS ,
▶hedhi huvurugika na zinaweza kutoka kwa muda mrefu,
▶Kuota nywele zisizohitajika na ovari kupanuka na kutofanya kazi vizuri,
▶Ugumba,
▶Mimba kutoka,
▶Kisukari type 2,
▶Unene,
▶Kansa ya Endometrial,
3. Congenital adrenal hyperplasia ( CAH )
Congenital adrenal hyperplasia (CAH),
Hili ni tatizo linalo athiri moja kwa moja adrenal glands na uzalishaji wa homoni mwilini.
CAH , Kwa hali nyingi mwili huzalisha androgen kupita kiasi.
Daliliza tatizo hili kwa wanawake ;
▶Ugumba,
▶Tabia za kiume,
▶Kuota nywele sehemu za siri mapema sana,
▶Chunusi nyingi.
BAADHI YA VYANZO VYA UPUNGUFU WA TESTOSTERONE KWA WANAUME.
Kadri mtu anavyozeeka, kiwango cha testosterone mwilini mwake hupungua hatua kwa hatua. Kupungua kwa asili hii huanza baada ya umri wa miaka 30 na inaendelea (karibu 1% kwa mwaka) katika maisha yake yote. Kuna sababu nyingine nyingi zinazosababisha testosterone kupungua ni pamoja na zifuatazo:
1. Kuumia (maumivu, kuingiliwa/kutatizwa usambazaji wa damu kwanye kende) au maambukizi ya kende (orchitis),
2. Matumizi ya dawa za kemikali kutibu saratani (Chemotherapy),
3. Matatizo ya mfumo wa utendaji kazi wa mwili (Metabolic) kama kuongezeka madini ya chuma mwilini (hemochromatosis),
4. Kutokufanya kazi vizuri tezi zinazotawala na kudhibiti utendaji kazi wa homoni zingine katika mwili (Pituitary grands),
5. Matumizi ya Dawa za Hospitali, pamoja na homoni zinazotumiwa kutibu saratani ya kibofu cha mkojo, na homoni kama vile (prednisone),
6. Magonjwa ya muda mfupi au sugu (ya muda mrefu),
7. Unywaji pombe,
8. Kovu tishu za ini (Cirrhosis of the liver),
9. Matatizo sugu ya figo hadi kupelekea kushindwa kufanya kazi,
10. Maambukizi ya VVU / UKIMWI,
11. Hali ya uchochezi kama (sarcoidosis) hali ambayo husababisha uvimbe wa mapafu na viungo vingine,
12.Maendeleo yasiyo ya kawaida ya tezi ya hypothalamus, (tezi katika ubongo ambayo inadhibiti homoni nyingi),
13. Klinefelter syndrome hali ya maumbile ambayo mwanaume huzaliwa nayo akiwa nakala ya ziada ya chromosomu ya X. Pia inaitwa syndrome ya XXY,
14. Viwango vya juu vya maziwa yanayozalisha homoni ya prolactini,
15. Unene au kupungua kwa uzito kupita kiasi,
16. Aina isiyodhibitiwa ugonjwa wa kisukari daraja la pili,
17. Kuzaliwa na kasoro (Inayotokea wakati wa kuzaa),
18 Kizuzi cha usingizi kisababishwacho na kushindwa kupumua kwa muda(Apnea a temporary cessation of brething),
19. uzee,
20. Upungufu wa estrojeni. (kawaida hutoka kwa chanzo cha nje au kimazingira),
21. Matumizi ya dawa za kunenepesha au kusisimua misuli,
22. Kukosekana msingi sahihi wa uzalishaji homoni zinazodhibiti mfumo wa utendaji kazi mwilini (Hypothyroidism),
23. Kuchelewa kubalehe,
24. Maumivu ya kichwa(Trauma),
25. Mfiduo wa mionzi au upasuaji wa ubongo uliotangulia,
BAADHIA YA NJIA ASILI ZA KUONGEZA KIWANGO CHA TESTOSTERONE.
▶Kupunguza uzito kwa wenye uzito uliopitaliza,
▶Kufanya mazoezi,
▶Kufanya mazoezi ya kujihami ya kuimarisha misuli,
▶Kulala vyakutosha,
▶Kupunguza msongo wa mawazo.
▶Kula vyakula vyenye alkaline
Uzindushi kwa wazazi , upungufu wa testosterone kwa wavulana wanao balehe unachangiwa vile vile na mfumo wa maisha ikiwemo lishe mbovo. chango la watoto ni chanzo kikubwa katika jamii zetu.
Mtaftie tiba/ufumbuzi mwanao haraka kwadalili hizi,(MUONE DAKTARI)
▶Tumbo kuuma,kuharisha, kusokota kukosa choo mara kwa mara,
▶Vidonda vya tumbo,
▶Kukosa hamu ya kula
▶Kuzubaa na kutokuwa mchangamfu
▶Maradhi kama sikosel , Sukari , Ngiri n.k
▶Huzuni na kutokuwa na furaha
▶Michezo ya hatari inayopelekea kuumia kende.
NJIA ZA KUDHITI UPUNGUFU WA TESTOSTERONE.
Hizi ni baadhi ya njia zilizotumiwa na wazee kuwakinga watoto na maradhi mbalimbali ikiwemo kuimarisha kinga ya mwili .
1. Mazoezi, mtoto apate muda wa kutosha wa kucheza,
2. Kila mwezi wape 10mls mafuta ya nyonyo ili kuondoa matatizo ya chango
(Kila kabila lina njia asili walizotumia kuondoa sumu mwilini na mlundikano wa taka vizuri kuwauliza upate kujua zaidi).
3. Wape watoto kila siku kimoja wapo ya hivi,(Hata wakubwa ni tiba nzuri kwao kwa Afya ya mwili kwa kuzifanya homoni ziwiyane ipasavyo)
A. Mafuta ya habat saudaa kijiko cha chakula 1x1 (mazuri sana ),
B. ASali kijiko kikubwa 1X1,
C. Mafuta ya zaytuni kijiko kikubwa (extra virgin)1X1,
D. Mafuta ya nazi kijiko kikubwa (extra virgin)1X1.
Kwa dalili au Ishara za upungufu wa testosterone muone daktari akufanyie uchungu kwa vipimo tatizo libainike nilipi.
MWANDISHI ABUU AJMI حفظه الله
________________________
Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia
+255758200163
+254743101242
DAR ES SALAM
TANZANIA.
🔴TUWEWAADILIFU USIBADILI CHOCHOTE KWENYE MAKALA HII.
▪️▫️◾️◽️◼️◻️⬛️◻️◼️◽️◾️▫️▪️
⛔️TAHADHARI CORONA IPO
⛔️EPUKA MIKUSANYIKO
⛔️NAWA MIKONO NA ACHA KUWAPA MIKONO WENGINE
💯TULIZANA NYUMBANI KAMA HUNA ULAZIMA WA KUTOKA