PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE.)
Pelvic Inflammatory Disease ( PID ) ni maambukizi katika viungo vya uzazi wanawake, yanayosababishwa na vimelea ama bakteria wanaosababisha magonjwa ya zinaa pindi hivyo vimelea ama bakteria wanapotoka katika mfumo wa mkojo na kwenda kuathiri viungo kwenye mfumo wa uzazi.
DALILI ZA PID.
▶Kupata maumivu wakati wa haja ndogo,
▶Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa,
▶Hedhi kuvurugiko,
▶Kutoa ute wenye harufu mbaya katika sehemu za siri na wenye rangi isiyo ya kawaida,
▶Kupata maumivu sehemu ya chini ya tumbo, au maumivu ya mgongo,
▶Homa,
▶Kutokwa damu(hedhi) baada ya tendo la ndoa,
▶Kuchoka sana ,
▶Mwili kuwa baridi,
▶Kukojoa mara nyingi,
▶Kupata maumivu makali ya vichomi wakati wa hedhi ,
▶Kutokwa na damu nyingi sana au vitone tone au muda mwingine damu kutoka zaidi ya mara moja ndani ya mwezi mmoja wa mzunguko,
▶Kutohisi njaa,
▶Kuhisi kichefuchefu na kutapika ,
▶Hedhi kupitiliza bila kutoka ,
Unaweza kuwa na PID na usipate dalili za hatari.
Kwa mfano, chlamydia inaweza kusababisha PID bila maumivu.
Wanawake ambao mimba hutunga nje ya mji wa uzazi (ectopic pregnancy) au wasio na uwezo wa kushika mimba hupata PID isababishwayo na chlamydia.
👉Ikumbukwe sio kila dalili tajwa hapo juu ni kwamba mtu ana PID laaa hasha bali kilicho sahihi ni mtu kufika kituo cha afya na kufanya vipimo pindi atakapokuwa na hizo dalili.
JINSI YA KUJIKINGA NA PID .
PID inaweza kutozuilika kwa sababu haisababishwi na bakteria wa zinaa pekee. Bacteria wa kawaida wanawza kusafiri hadi katika viungo vya uzazi na kusabibisha PID.
Kinga ni kukiepusha na haya,
~Kuacha kusafisha uke kwa sabuni,
~Kushiriki tendo la ndoa na watu tofauti tofauti,
~Kutumia Njia za kupanga uzazi kama IUS au IUD (Kutumia kiplastic kidogo chenye umbo la T kipandikizwacho katika kizazi na daktari au nesi kuzuia mimba kutunga)
~Kusafisha kizazi,
~Kulewa chakari kunapelekea kufanya maasi yanayopelekea maambukizi,
Kuepuka PID ni vyema kuepuka hayo tuliyotaja hapo juu. Muone Daktari haraka iwezekanavyo kwa dalili ndogo au chache ufanyiwe vipimo na Tiba hali ikiwa changa, bacteria hajadhiri viungo vingi vya uzazi .
WANDISHI ABUU NAWFAL MZAMIRU KATUNZI NA ABUU AJMI .
________________________
Kwa Tiba na Ushauri wasiliana na Subira Tiba Asilia
+255758200163
+254743101242
DAR ES SALAM
TANZANIA.
🔴TUWEWAADILIFU USIBADILI CHOCHOTE KWENYE MAKALA HII.
▪️▫️◾️◽️◼️◻️⬛️◻️◼️◽️◾️▫️▪️
No comments:
Post a Comment