Thursday, July 2, 2020

MAFUTA YA NAZI HUPUGUZA KUPANUKA TEZI DUME

*TAFITI KUBAINI ATHARI YA MAFUTA YA NAZI KTK UVIMBE WA TEZI DUME UNAOSABABISHWA NA HOMONI YA KIUME,KUPITIA PANYA(sprague Dawley)*

Kabla ya kutoa tarjama ,ntangulize maelezo haya ;

>Tafit/majaribio mengi za binadamu wanatumika wanyama wanaokaribia mfanano wa kimwili mfano Sungura ,panya nk

>Kila mwanaume ana tezi dume na kazi yake huwa ni kuzalisha majimaji mepesi,hutoka pamoja na manii .

>Tezi dume si korodani(kende).
> kende huzalisha mbegu(manii) na Tezi duma majimaji tu .

>kuhusu Uvimbe wa Tezi ,hakuna sababu maalum inayojulikana  lkn kuna nadharia(theories) . Imeonekana uvimbe husababishwa homoni ya kiume "Dihydrotestosterone (DHT)" ,ambayo hutokana Testosterone(TS) inayozalishwa na korodani .
>Tunahitaji TS ,lkn kuna  enzyme (5alpha reductase) hubadilisha kuwa DHT .

>Hospitalin watu wenye uvimbe hupewa 'Finasteride' dawa ambayo huzia huyu enzyme asibadili TS -->DHT .

*UTAFITI* ;

Uvumbe wa tezi dume(BPH) hutokea pindi tezi hii hukua kwa kasi(hyperplasia) na kupelekea ugumu wa mkojo kupita.

Kuna mafuta aina ya SPLE yamekuwa yakitumika kutibu uvimbe huu ,kwani nayo huzuia enzyme (5reductase) kubadili TS --->DHT .Tunajua DHT ndio husababisha Uvimbe.
Mafuta haya ya SLPE yana lauric, myristic and oleic acids  .Mafuta ya nazi nayo yana lauric acid na myristic acid kama SLPE.
Hivyo basi tukachunguza Mafuta ya Nazi kubaini kama nayo yataweza kutibu/kupunguza Uvimbe.

Tukatumia makundi 7 kila moja likiwa na panya 10.
Kundi 1 tunakalipa mafuta ya soya na makundi 6 yalobaki tunakayapa homoni ya kiume ili kukuza kwa kasi tezi dume zao .


Baada ya muda tukaanza matibabu kwa muda wa siku 14. Baadhi wakatibiwa kwa mafuta ya SLPE na baadhi kwa Mafuta ya nazi na baadhi kwa mafuta ya alizeti .

Baada ya muda tukawaua na kutazama ukubwa/uzito wa tezi dume zao .Majibu yakawa hivi Wale walotibiwa kwa mafuta ya SLPE na NAZI inakaonekana tezi dume zao kupungua sana uzito kwa asilimia 61.5% na 85% .

Hitimisho ; Imethibitisha mafuta ya Nazi yana punguza uvimbe wa Tezu dume ,hii ni kwa sababu yana lauric na myristic  acids ambazo huzia DHT kutengenezeka.


NIMEJARIBU KUFUPISHA MAELEZO ILI KUPATA MAUDHUI.

Maoni ;

>Kuna uelewa upo mtaani ,juu NAZI /MADAFU kuwa yanahusisha na tatizo la BUSHA ,Si kweli . Hakuna uhusiano ,busha zinasabishwa na filarias wanaonezwa na aina ya mbu ,na mbu hawa hupatikana baadhi ya maeneo mf;pwani.

>Kuna tofauti ktk Saratani ya Tezi dume na Uvimbe huu .
Kuhusu saratani ya Tezi hii inasemekana ulaji wa nyama nyekundu,Maziwa , sigara na pombe vinahusishwa nayo lkn hakuna ushahid wa kutosha .


Barakallahu fiikum.




IMEANDALIWA NA ABAA MAYSARAH ,MD. حفظه الله

________________________


kwa tiba na ushauri wasiliana na subira tiba Asilia .

https://t.me/Subratibaasilia


+255 75800163.

+254 743101242.

DAR ES SALAM .

TANZANIA .

TUWE WAADILIFU USIBALI CHOCHOTE KWENYE MAKALA HII.

No comments:

CHANGO

CHANGO . watu wengi wanauliza chango ni nini ?  Chango ni jina la kiswahili lipatikanalo kwa baadhi ya makabila ya kibantu. Maana ya chango ...