CHANGO .
watu wengi wanauliza chango ni nini ?
Chango ni jina la kiswahili lipatikanalo kwa baadhi ya makabila ya kibantu.
Maana ya chango ni mjumuiko maradhi ya tumbo (mfumo wa usagaji chakula ) na mfumo wa uzazi .
AINA ZA MACHANGO .
1. CHANGO LA NGIRI ,
Ni mjumuiko wa maradhi ya tumbo na uzazi kwa asilimia kubwa kwa jinsia kiume .
Ngiri ni hali ya utumbo kushindwa kujishikiza katika kuta zake na kupenya sehemu dhaifu ya tumbo na kupenyeza sehemu isiyokuwa yake ya asili na kutuna katika kitovu au kupenya na kuingia sehemu ya korodani hii inajumuisha matumbo kusokota na kuuma sana, kukosa choo na miwasho sehemu za siri (bawasiri), kwenye mapaja na nyuma ya muundi .
Kwa mwanamke ngiri ni maradhi ya tumbo ambayo haswa huwa femoral hernia.
Kinyume na femoral hernia mwanamke haingi katika maradhi ya ngiri bali itsemwa ana chango .
Misokoto ya tumbo ya watoto ujumla wake huitwa chango la watoto ikiwa ni pamoja na kukosa choo . Ikidhibitika utumbo umepenya katika kuta za tumbo itaitwa ngiri ima ngiri ya kitovu,ngiri maji au zinginezo .
Maradhi kama busha, tezi dume, uti,pid na maradhi ya ngono sio katika chango.
2. CHANGO LA UZAZI
A. KIGUMA/FUNGASI.
Kiguma au fungus zinazo kusudiwa katika tiba asilia ni fungus za kwenye kizazi na za tumboni .
B. UVIMBE KWENYE KIZAZI/KUZIBA MIRIJA YA UZAZI
Hizi ni vimbe viotazo nje au ndani ya kizazi au katikati ya kuta za kizazi au katika mirija ya uzazi , au mirija ya uzazi kuziba au kujaa maji kizazi au kuta za kizaza kunenepa hutambulika kama chango
B. HEDHI KUVURUGIKA
Chango hili linajumuisha maumimu kabla au wakati au baada ya hedhi,
kuosa hamu ya tendo la ndoa na kutoshika ujauzito.
Hedhi kuvurugika kutoka kwa wingi sana au chache , kutoka zaidi ya mara moja kwa mwezi au kutokutoka kabisa hizi zote ni dalili ya chango la uzazi.
C . MAYAI KUTOPEVUKA
Mayai ya mwanamke kukosa uwezo wa kupevuka na kushika ujauzito au mimba kushika na kutoka au mimba kutunga nje ya kizazi.
3. CHANGO LA SIHIRI.
Chango la sihiri linajumuisha maradhi yatokanayo na sihiri ya tumboni na viungo vya uzazi ambayo asili yake ni sihiri ima ni jini au uchawi .
mfano wa dalili za chango la sihiri, matatizo ya tumbo au uzazi ambayo katika vipimo vya hospitali tatizo halionekani japo mgojwa anamaradhi au kapata dalili haswa za sihiri .
Dalili za chango zitategemea na aina ya chango husika.
Uhalisia chango ni haswa kwa maradhi ya wanawake ya uzazi. wanaume itaitwa chango la ngiri hatakama sehemu ya utumbo haijatokeza nakupenya katika sehmu dhaifu.
IMEANDALIWA NA ABUU AJMI
________________________
kwa tiba na ushauri wasiliana na subira tiba Asilia .
https://t.me/Subratibaasilia
+255 75800163.
+254 743101242.
DAR ES SALAM .
TANZANIA .
TUWE WAADILIFU USIBALI CHOCHOTE KWENYE MAKALA HII.